Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 06:36

Walimu waandamana kupinga utawala wa kijeshi Sudan

Wasudan wakiimba nyimbo wakati wa maandamano dhidi ya jeshi mjini Khartoum.
Wasudan wakiimba nyimbo wakati wa maandamano dhidi ya jeshi mjini Khartoum.

Vikosi vya usalama vya Sudan siku ya Jumapili vilitumia gesi ya kutoa   machozi katika maandamano ya kupinga mapinduzi yaliyofanywa na  kundi la walimu mwanzoni mwa mgomo wa siku mbili kupinga jeshi kujitwalia madaraka  mwezi uliopita.

Darzeni ya walimu walibeba mabango yenye maandishi "hapana, hapana kwa utawala wa kijeshi" na kutoa wito wa mabadiliko ya utawala kamili wa kiraia katika maandamano nje ya wizara ya elimu katika mji mkuu Khartoum.

Maandamano ya kupinga mapinduzi ya nchi nzima ikiwa yaiyofanywa na maelfu ya watu Oktoba 30 yametokea tangu mapinduzi ya Oktoba 25 lakini yamekabiliwa na ukandamizaji mbaya. Takriban waandamanaji 14 wameuawa na kiasi cha 300 kujeruhiwa, kulingana na Kamati Kuu huru ya Madaktari wa Sudan.

Tulipanga msimamo wa kimya kimya dhidi ya maamuzi ya Burhan nje ya wizara ya elimu, alisema Mohamed al-Amin, mwalimu wa jiografia ambaye alishiriki katika maandamano hayo dhidi ya Jenerali mkuu wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Burhan.

Polisi walikuja baadaye na kuturushia gesi ya kutoa machozi ingawa tulikuwa tumesimama tu barabarani na kubeba mabango,” alisema.

Hakuna ripoti za mara moja za majeruhi lakini umoja wa walimu wa Sudan ulisema idadi kubwa ya walimu walitiwa ndani.

XS
SM
MD
LG