Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:11

Maafisa wa usalama Sudan wawatawanya waandamanaji


Wapinzani wa mapinduzi ya kijeshi ya Sudan waandamana kaskazini mwa Khartoum huku polisi waliwafyetulia mabomu ya kutoa machozi, Nov. 13, 2021.
Wapinzani wa mapinduzi ya kijeshi ya Sudan waandamana kaskazini mwa Khartoum huku polisi waliwafyetulia mabomu ya kutoa machozi, Nov. 13, 2021.

Maafisa wa usalama wa Sudan wamefyatua gesi ya kutoa machozi dhidi ya maelfu ya waandamanaji katika sehemu mbali mbali za nchi hiyo, siku mbili baada ya jeshi kujaribu kuimarisha utawala wake kwa kuunda baraza jipya la utawala. 

Maandamano hayo ya kuunga mkono demokrasia yanafanyika karibu wiki tatu baada ya Jenerali Abdel Fatah al-Burhan kuipindua serikali, kuwafunga baadhi ya viongozi wa kiraia na kutangaza hali ya dharura nchini.

Licha ya kufungwa kwa mawasiliano yote ya mtandao, mamia ya watu walikusanyika katika mji wa Ondurman karibu na mji mkuu wa Khartoum ambako polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.

Katika mji mkuu, Mohieddine Hassan ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu wanakusanyika pamoja kuupinga utawala wa kijeshi.

Maandamano hayo yamefanyika licha ya kuongezwa kwa wanajeshi, polisi na wanamgambo katika sehemu mbali mbali za Khartoum na daraja na barabara muhimu kufungwa.

Hatua ya jeshi kuchukua tena madaraka Oktoba 25 ilishutumiwa vikalo kote duniani pamoja na kulaaniwa kukandamizwa kwa waandamanaji barabarani wanaotaka mfumo wa kidemokrasia udumishwe nchini mwao.

Umoja wa mataifa umetoa wito kwa maafisa wa usalama kujizuia kutumia nguvu , kwani tangu kutokea mapinduzi karibu watu 15 wameuwawa kulingana na chama huru cha wafanyakazi wa afya.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG