Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:50

Washington kuisaidia Niger kupambana na uasi


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (katikati) akiondoka kuelekea Niger kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 16 Machi 2023. Picha na TIKSA NEGERI / POOL / AFP.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (katikati) akiondoka kuelekea Niger kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 16 Machi 2023. Picha na TIKSA NEGERI / POOL / AFP.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaitembelea Niger kituo chake cha pili kutembelea mataifa ya Afrika. Anatarajiwa kutangaza msaada zaidi wa Marekani kwa Niger katika mapambano dhidi ya uasi wa wanajihadi ambao umewalazimisha mamilioni ya watu kukimbia makazi yao huko Sahel.

Wakati akiwa nchini Ethiopia Blinken alikutana na viongozi wa juu katika juhudi za kurekebisha uhusiano ulioharibika baada ya vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili dhidi ya majeshi katika mkoa wa kaskazini wa Tigray ambapo takriban watu 500,000 walipoteza maisha. Ikilenga sera ya amani na kuhamaisha haki, ambayo itasimamia uwajibikaji kwa ukatili uliotendwa na pande zote katika mzozo, ni mambo ambayo yalikuwa juu katika ajenda.

Sherehe ya kitamaduni ya kunywa kahawa ilikuwa ni mwanzo mzuri kwa mikutano ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na maafisa wa juu wa serikali na viongozi wa Tigray mjini Addis Ababa huku pande zote zina na hamu kubwa ya kurekebisha mahusiano yaliyoingia dosari kutokana na miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Blinken alichukua muda kuangalia jinsi maisha ya watu walivyopotea na maumivu ambavyo watu wameyapata.Mzozo huu kwa hakika ulikuwa na athari mbaya. Maelfu ya watu waliuawa. Manyanyaso ya kingono dhidi ya wanawake yalisambaa. Mamilioni ya watu walikimbia makazi yao. Wengi waliachwa wakiwa na shida ya chakula, makazi, dawa. Mahospitali, shule na biashara zilipigwa mabomu na kuharibiwa. Mkataba wa kusitisha mapigano ni mafanikio makubwa na hatua moja mbele katika kuokoa maisha na kubadili maisha. Bunduki zilikuwa kimya. Wakapita mapigano yaliposimama, ukiukaji wa haki za binadamu nao ulishuka.”

Blinken alisema uongozi wa kiafrika, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na viongozi wa Tigray wanastahili pongezi kwa kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwezi Novemba, wakiungwa mkono na Marekani. Alifikisha baadhi ya habari nzuri, na kuelezea kwamba Marekani ni mfadhili mkubwa sana wa misaada kwa Ethiopia.

“Hivi leo, natangaza msaada wa ziada wa dola milioni 331 kwa ajili ya chakula na misaada ya kibinadamu ambayo itawafikia mabilioni ya watu, mamilioni ya waathirika wa mzozo nchini Ethiopia, na wale walioathiriwa na ukame.”

Mtalaamu mmoja ameiambia VOA kwamba kurejesha uhusiano wa pamoja wa kawaida baada ya vita vya kikatili itakuwa ni mchakato na siyo jambo ya kuwasha na kuzima, lakini Marekani iko katika nafasi isiyo ya kawaida kusaidia.

Joseph Siegle wa Kituo cha Afrika cha Masuala ya Mkakati anasema “Nadhani hapo ndipo Marekani ina jukumu muhimu sana kama mshirika anayeaminika, na mdhamini. Inaweza kuhakikisha kwamba maslahi ya watigray wanafikiriwa wakati pande zote zikisonga mbele. Wanaweza kuhakikisha kwamba uhuru wa Ethiopia na maslahi ya Ethiopiapia yanaheshimiwa.”

Mtalaamu mwingine ameiambia VOA kwamba Abiy ana hamu kubwa kurejesha uhsuiano wa kawaida na kurejea kwenye program ya Marekani ya biashara , lakini ameomba kuwepo na tahadhari.

Sarah Yager wa Human Rights Watch anasema “Kwa hiyo, alichokuwa anakifanya ni kupuuza ukatili ambao ulitokea uliofanywa na pande zote zilizokuwa zinagombana, lakini pia zake mwenyewe, kwa maelekezo yake katika sehemu kama vile Tigray. Hivyo anachoangalia ni kupata ahueni ya kiuchumi kutoka Marekani. Anaangalia kupata washirika wengine kote duniani ambao watakuwa na hamu ya kuwa mataifa fadhili, na kuwa katika biashara huru na kuzirejesha biashara nchini Ethiopia.”

Blinken alisema wakati amani inaendelezwa, Ethiopia inaelekea kwenye upande sahihi, na Marekani inashirikiana utashi wake, lakini haiko tayari kuikaribisha tena kwa sasa katika program ya biashara ya Marekani.

XS
SM
MD
LG