Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:47

Mkutano wa G-20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje washindwa kuafikiana juu ya vita vya Russia na Ukraine


Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G-20 walishindwa kufikia maridhiano kuhusu tofauti zao kuhusiana na uvamizi wa russia nchini Ukraine walipokutana  Alhamis nchini India.

Waziri wa mambo ya nje wa India, S. Jaishankar aliwaambia wanahabari kuwa mgawanyiko ulilizuia kundi hilo kuwa na taarifa ya pamoja, na kuelezea maoni tofauti sana ya baadhi ya nchi kuhusiana na mzozo huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya nje wa Russia, Sergey Lavrov, na mwenzao wa China, Qin Gang, ni miongoni mwa wale ambao walikuwepo New Delhi.

Afisa mwandamizi wa Marekani aliwaambia wanahabari kwamba Blinken alikutana na Lavrov pembeni ya mkutano huo wa Alhamisi, na kusisitiza kwamba Marekani iko tayari kuiunga mkono Ukraine, kujitetea katika mzozo huu ambazo umekuwa na uharibifu mkubwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG