Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:21

Blinken asema Russia haiwezi kuachiwa iendeshe vita Ukraine bila ya kuwajibishwa


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Ijumaa, baada ya kukutana na wenzake wa India, Japan na Australia, kuwa Russia haiwezi kuachiwa iendeshe vita bila ya kuwajibishwa

Wanachama wa kikundi kinachoitwa Quad walikutana pembeni ya mkutano ya G-20 unaofanyika huko New Delhi.

Kikundi cha Quad kilitoa taarifa kikisema kuwa tishio la Russia la matumizi ya silaha za nyuklia “halikubaliki.”

Mwezi uliopita, Rais wa Russia Vladimir Putin alisitisha mkataba wa silaha za nyuklia na kuitishia Ukraine kwa silaha za nyuklia.

Makampuni ya ulinzi ya Russia yanaonyesha bidhaa zao katika maonyesho makubwa ya kimataifa ya silaha, wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema Ijumaa katika maelezo yake ya kila siku juu ya uvamizi wa Russia huko Ukraine.

Makampuni hayo yanatangaza mfumo wa ulinzi aina ya Arena-E au APS ambao wizara hiyo ilisema umeundwa ili kuboresha ulinzi wa magari yenye silaha.

Maelezo ya bidhaa za APS zinazotangazwa katika maonyesho ya hivi karibuni yanaeleza kuwa APS “inaondoa hatari ambazo ni kubwa zaidi zilizokuwa zinayakabili magari yenye silaha.”

Hakuna ushahidi, hata hivyo, kuwa mfumo huo umeshawekwa katika magari ya Russia huko Ukraine, ambapo imepoteza zaidi ya magari 5,000 yenye silaha, kwa mujibu wa wizara hiyo

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG