Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:19

Mkuu wa jeshi la mamluki la Russia Wagner atajwa kuwa mhalifu wa kivita.


Mfanyabiashara wa Russia na mwanzilishi wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin akitazama mbele ya mkutano na Rais wa Russia Vladimir Putin na mwenzake wa China Xi Jinping.
Mfanyabiashara wa Russia na mwanzilishi wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin akitazama mbele ya mkutano na Rais wa Russia Vladimir Putin na mwenzake wa China Xi Jinping.

Mwanasheria mkuu wa Marekani siku ya Jumatano alimtaja Yev-geny Prig-ozhin mkuu wa jeshi la mamluki la Russia Wagner linalopigana nchini Ukraine kuwa ni  mhalifu wa kivita.

Mwanasheria Mkuu Merrick Garland alikiambia kikao cha Seneti kwamba wizara ya Sheria inaisaidia Ukraine kuchunguza uhalifu wa kivita unaodaiwa kufanywa tangu uvamizi wa Russia ikiwa ni pamoja na kundi la kijeshi la Wagner.

Bwana Prig-ozhin, ambaye anashughulikia suala hilo, kwa maoni yangu ni mhalifu wa vita, Garland aliambia kikao hicho.

Labda hiyo haifai kwa mimi kusema kama jaji kabla ya kupata ushahidi wote. Lakini nadhani tuna ushahidi wa kutosha kwa wakati huu kwangu kuhisi hivyo.

Kundi hilo, ambalo linahusika na mashambulizi dhidi ya Waukraine katika mkoa wa Donbass, ikiwa ni pamoja na kuwaleta wafungwa kutoka katika magereza ya Russia ni jambo lisiloeleweka wanalolifanya.

XS
SM
MD
LG