Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:19
VOA Direct Packages

Macron aanza ziara ya mataifa manne barani Afrika


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba mjini Paris. Feb. 27, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba mjini Paris. Feb. 27, 2023.

Rasi wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumatano ameanza ziara ya mataifa manne barani Afrika, wakati kukiwa na kampeni kali ya kupinga taifa lake, iliyopelekea kuondolewa kwa vikosi vyake kutoka Mali na Burkina Faso hivi karibuni. Ziara hiyo itampeleka Gabon, Angola, Jamhuri ya Congo na DRC.

Siku chache kabla ya kuanza ziara yake, Macron alisema kwamba Ufaransa ingechukua mwelekeo tofauti katika uhusiano wake na bara la Afrika, kwa kuwa na unyenyekevu mkubwa. Kama mojawapo ya mbinu mpya katika mkakati huo, vituo vya kijeshi vya Ufaransa barani humo vitageuzwa kuwa vya mafunzo ya kijeshi wakati baadhi, hatimaye vitaendeshwa kwa ushirikiano na mataifa ya Afrika. Miongoni mwa mataifa anayotembelea, Gabon na Jamhuri ya Congo yalikuwa koloni za Ufaransa.

Kujitenga kwa Ufaransa na mataifa ya kiafrika kulitoa nafasi kwa makundi mengine kupenya kama lile la kijeshi la Russia la Wagner ambalo limekita mizizi nchini Mali na kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako linalaumiwa kutekeleza ukatili kama vile mauaji ,ubakaji na mateso. Vifo kutokana na makundi ya kigaidi barani Afrika viliongezeka kwa karibu asilimia 50 mwaka jana na kufikia zaidi ya 19,000 hasa magharibi mwa Sahel kulingana na ripoti kutoka kituo cha masomo maalum cha Afrika

Hata hivyo kwenye hotuba yake, Macron alisema kwamba taifa lake halitakubali kulaumiwa kutokana na kudorora kwa hali ya usalama nchini Mali, wala kukubali Ufaransa itumike kama kisingizio.

XS
SM
MD
LG