Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:59

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani aitaka Russia na China kuunga mkono juhudi za kuleta amani Ukraine


Wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Kharkiv, Ukraine, Alhamisi, Februari 23, 2023. Picha na AP/Vadim Ghirda, Maktaba.
Wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Kharkiv, Ukraine, Alhamisi, Februari 23, 2023. Picha na AP/Vadim Ghirda, Maktaba.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Jumatano alielezea wasi wasi wake kuhusu jinsi gani Russia na China watafanikisha amani nchini Ukraine, akitaja ukosefu wa hatua madhubuti zinazoonyesha uungaji mkono kauli zinazohusu juhudi za kuleta amani.

Akizungumza katika ziara yake nchini Uzbekistan, Blinken aliwaambia waandishi wa habari kwamba kama Russia watajihusisha katika njia ya kidiplomasia kwa dhati ili kumaliza uchokozi wake, basi Marekani haraka itaingia na kujihusisha katika juhudi hizo.

Lakini alisema hatua za Russia, ikiwa pamoja na matakwa ya Rais Vladimir Putin kwamba Ukraine itambue udhibiti wa Russia katika maeneo ya ardhi ya Ukraine, inaonyesha Russia haitaka kutumia njia hiyo.

“Swali la msingi endapo Russia itafikia mahala ambapo iko tayari kwa dhati kabisa kukomesha uchokozi wake kwa njia inayoendana na kanuni na misingi ya Umoja wa Mataifa.”

“Hakuna anayetaka amani haraka zaidi kama watu wa Ukraine. Wao kila siku ni waathirika wa uchokozi wa Russia,” alisema Blinken. “Sote tunajua ukweli kwamba vita vinaweza kumalizika kesho, au leo, endapo Rais Putin ataamua. Amevianzisha, anaweza kuvimaliza.”

Blinken alisema pendekezo la amani lililotolewa na China lina vipengele vizuri, ambavyo baadhi yake viko katika mpango wa amani wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy mwenyewe.

Lakini Blinken alisema endapo China ina nia ya dhati kuhusu wito wake wa kutaka uhuru wa mataifa yote uzingatiwe, basi ingetumia kipindi cha mwaka jana kuunga mkono uhuru kamili wa Ukraine katika kukabiliana na uvamizi wa Russia

XS
SM
MD
LG