Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 18:40

Blinken atangaza msaada mpya kwa Ethiopia zaidi ya dola milioni 331


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken

Ufadhili huu utatoa msaada wa kuokoa maisha kwa wale waliokimbia makazi yao na kuathiriwa na mzozo, ukame, na ukosefu wa chakula nchini Ethiopia

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken ametangaza zaidi ya dola milioni 331 msaada mpya wa kibinadamu kwa Ethiopia katika mwaka wa fedha wa 2023 kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Ufadhili huu utatoa msaada wa kuokoa maisha kwa wale waliokimbia makazi yao na kuathiriwa na mzozo, ukame, na ukosefu wa chakula nchini Ethiopia. Msaada huu unajumuisha dola milioni 12 kupitia Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje inayohusika na Idadi ya Watu, Wakimbizi na Uhamiaji na zaidi ya dola milioni 319 kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa.

Hii inafanya jumla ya msaada wa kibinadamu wa Marekani kwa ajili ya eneo hilo kuwa zaidi ya dola milioni 780 katika mwaka wa fedha wa 2023. Marekani ni mfadhili mkubwa wa moja ya misaada ya kibinadamu nchini Ethiopia. Msaada wetu hutoa msaada muhimu, wa kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, maji salama ya kunywa, usafi wa mazingira na juhudi za huduma za afya, elimu, na huduma zingine muhimu. Tangazo hili litasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na Afrika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG