Zaidi ya watu 440 wamekufa na juhudi za kuwasaka wengine 63 ambao hawajulikani walipo zinaendelea.
Baadhi yao wanasadikiwa walichotwa na maji ya mito na maporomoko ya matope.
Serikali imetangaza jimbo la Kwazulu -Natal kuwa eneo la janga.
Maafisa wanaeleza mafuriko hayo kuwa ni makubwa kuwahi kutokea katika jimbo hilo.
Waziri Mkuu wa Kwazulu –NATAL , Silhe Zikaka amesema kuwa karibu nyumba 4,000 zimebomolewa na nyingine zaidi ya 8,000 zimeharibiwa nyingi katika mji wa Durban na maeneo yanayozunguuza eneo hilo.
Wote polisi na jeshi walihusika katika juhudi za kuwatafuta watu ambapo miili sita zaidi imepatikana Jumapili, vyombo vya habari vinaripoti.
Waziri Mkuu wa Kwazulu-Natal anasema:“Kwa upande wa kazi ya utafutaji na uokoaji, hali mbaya ya hewa ya sasa imepunguza kasi ya tathmini ya shughuli za uokoaji katika eneo.
lakini kwa mara nyingine tumerejea leo asubuhi, Kwazulu Natal ilipokea simu 38 kwenye matukio ambayo tulikwenda, miili ya watu sita iliopolewa. Tunasimamia idadi ya watu 63 ambao hawajulikani walipo . idadi hiyo sasa ni 443.