Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:30

Idadi ya vifo Afrika kusini yafikia 259


Mafuriko katika jimbo la KwaZulu Natal, Afrika kusini
Mafuriko katika jimbo la KwaZulu Natal, Afrika kusini

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ameahidi kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko ambayo yameua zaidi ya watu 259, kusababisha uharibifu mkubwa na kutatizo shughuli katika mojawapo ya bandari yenye shughuli nyingi sana barani Afrika.

Ramaphosa ametembelea familia za watu waliopoteza wapendwa wao katika jimbo la Zulu-Natal, ikiwemo familia iliyopoteza watoto wanne baada ya mafuriko kusomba nyumba yao.

Ramaphosa ameambia familia hizo kwamba japo mioyo yao inahisi uchungu mkubwa wa kupoteza wapendwa wao, serikali yake itafanya kila iwezekanalo kuwasaidia, na kwamba anaomboleza pamoja nao.

Mvua kubwa iliyonyesha jumatatu, iliharibu nyumba, barabara na kupelekea watu kadhaa kukoseshwa makazi.

Mvua inatarajiwa kuendelea kunyesha katika sehemu za pwani za mkoa huo.

Jeshi la Afrika kusini linaendelea kutoa msaada kwa kutumia helikopta katika sehemu ambazo usafiri umeharibika kabisa baada ya barabara kusombwa na mafuriko hayo.

XS
SM
MD
LG