Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 01:52

Mvua zaidi zakumba mashariki mwa Afrika Kuisni ambako mafuriko yamesababisha maafa makubwa


Mtu kasimama kwenye lori lililokwama kwenye maji ya mafuriko katika mji wa Ladysmith, KwaZulu Natal, Afrika Kusini.
Mtu kasimama kwenye lori lililokwama kwenye maji ya mafuriko katika mji wa Ladysmith, KwaZulu Natal, Afrika Kusini.

Jimbo la kusini mashariki mwa Afrika Kusini linalokabiliana na mafuriko makubwa, limepata mvua nyingi Jumamosi baada ya kukumbwa na dharura kali kuwahi kutokea katika jimbo hilo, lililosababisha vifo vya karibu watu 400 wiki hii.

Mafuriko makubwa yamekumba sehemu ya mji wa mashariki wa Durban, wiki hii yakiharibu barabara, hospitali na kusomba nyumba na watu walokwama.

Huduma za dharura katika jimbo la kusini magharibi la KwaZulu-Natal ziko katika hali ya juu ya tahadhari baada ya wataalamu wa hali ya hewa kutabiri kuwepo kwa mvua nyingi mwishoni mwa wiki hii ya Pasaka.

Taarifa ya serikali iliyotolewa Jumamosi inaeleza kwamba idadi ya vifo hivi sasa ni 398 na watu 27 hawajulikani waliko, kufuatia dharuba na mvua za wiki nzima.Taarifa hiyo inaeleza kwamba hospitali na zahanati 58 zimeharibika vibaya sana.

Kazi za huduma za dharura na uwokozi zinaendelea katika jiji la Durban lenye wakazi milioni 3.5, jiji ambalo lingekua linasherehekea siku kuu ya Pasaka.

Hata hivyo msemaji wa huduma za dharura za Afya Robert McKenzi anasema haimkiniki hivi sasa siku sita baada ya kutokea mafuriko ya kwanza kuweza kumpata mtu hai.

Mafuriko yameharibu kwa sehemu fulani karibu nyumba 13, 500 na kuharibu kabisa karibu nyumba 4,000.

Maafisa wa jimbo wamewahimiza watu wanaoishi katika maeneo yenye hatari kuhama na kwenda katika shule na majumba ya umaa.

XS
SM
MD
LG