Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:36

Bandari ya Afrika Kusini yafungwa baada ya mafuriko


Watu wamekwama kuvuka wakiwa mbele ya daraja ambalo lilichukuliwa na maji baada ya mvua na mafuriko yaliyoendelea huko Ntuzuma, nje ya Durban, Afrika Kusini. (Picha na AP)>
Watu wamekwama kuvuka wakiwa mbele ya daraja ambalo lilichukuliwa na maji baada ya mvua na mafuriko yaliyoendelea huko Ntuzuma, nje ya Durban, Afrika Kusini. (Picha na AP)>

Usafirishaji bidhaa Afrika Kusini katika bandari yenye harakati nyingi umeahirishwa kutokana na mafuriko katika jimbo la kwazulu –Natal ambalo hadi sasa kuna vifo vya watu 59.

Mafuriko yameharibu, madaraja, na nyumba baada ya mvua ya miezi mitano kunyesha kwa siku tatu tu.

Kampuni inayomilikiwa na serikali, Transnet inasema bandari ya DURBAN imefungwa hadi itakapotangazwa tena baadae, kwa sababu ya uharibifu wa mazingira uliotokana na mafuriko.

Barabara kuelekea katika eneo hilo zimeharbiwa vibaya na hazipitiki.

Ghala ya kuhifadhi makontena karibu na barabara kuu yenye harakati nyingi imekumbwa na mafuriko mabaya na mamia ya makontena yalichotwa na maji.

Mji wa DURBAN umekuwa kitovu cha janga la asili ambalo linabadilika haraka na kuwa mzozo wa kibinadamu.

XS
SM
MD
LG