Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 20:59

Wamarekani wenye asili ya Kenya washtakiwa kwa ugaidi Michigan


Uwanja wa ndege wa Michigan

Wamarekani watatu wenye asili ya Kenya wamefunguliwa mashtaka kwa madai ya kula njama ya kuwasaidia kikundi cha Islamic State.

Wanaume hao walikamatwa uwanja wa ndege wa Michigan na hatimaye mpango huo kudhibitiwa, vyombo vya usalama vimetangaza Jumanne.

Wote wakiwa katika umri wa miaka 20 na wanauhusiano wa kindugu, inadaiwa walijirikodi katika picha za video wakitoa ahadi kuwa waaminifu kwa kikundi cha IS.

FBI iliwasiliana nao

Walizungumza juu ya uwezekano wa kutumia gari kushambulia nchini Marekani, iwapo mmoja wao hataweza kusafiri nje ya nchi kuungana na kikundi hicho cha kigaidi katika mapigano yake.

Wafanyakazi wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai, FBI, waliwapeleka askari kanzu kuzungumza na watuhumiwa hao na vibali vya upekuzi kadhaa vilitolewa kupekuwa akaunti zao za mitandao ya kijamii ikiwa ni hatua ya kufuatilia mawasiliano ya washukiwa hao kati yao wenyewe, kwa mujibu wa waraka wa kiapo uliofikishwa katika mahakama ya serikali kuu.

Wote watatu walikamatwa siku ya Jumatatu wakiwa uwanja wa ndege wa Gerald Ford Airport katika jiji la Grand Rapids, jina la mmoja wao ni Muse Abdikadir Muse, 23, ambaye pia anajulikana kama Muse Muse, wakati akiwa anapita katika dawati la upekuzi wa abiria kwa ajili ya mchakato wa kiusalama, TSA.

Vyombo vya usalama vimesema kuwa alikuwa amepita katika dawati hilo kwa ajili ya safari ambayo hatimaye ingempeleka hadi Mogadishu, Somalia kwa lengo la kujiunga na kikundi cha IS.

Katika kubadilishana mawasiliano katika mitandao ya kijamii na mpelelezi wa FBI, Muse anadaiwa kuwa alikuwa anataka kujiunga na kikundi cha IS huko Somalia na “kwenda kupigana mstari wa mbele,” kwa mujibu wa waraka huo wa kiapo.

Wakamatwa uwanja wa ndege

Polisi pia wamemkamata uwanja wa ndege watu ambao ni washirika wa Muse katika njama hiyo ya kufanya vitendo hivyo vya ugaidi : Kaka yake Mohamud Abdikadir Muse, 20, na ndugu mwengine, Mohamed Salat Haji, 26.

Wawili hao wanadaiwa kuwa walinunuwa tiketi ya ndege na kumpeleka Muse uwanja wa ndege.

Wanaume hao watatu, ambao walichukua uraia wa Marekani asili yao ni Kenya, wameshtakiwa kwa kula njama kutoa msaada au fedha kwa taasisi ya kigaidi ya nje.

Vyombo vya usalama vilikuwa na umuhimu na kaka ya ndugu hao, Muse, kuanzia mwezi April 2016, wakati ikidaiwa kuwa aliposti waziwazi ujumbe wa kuwaunga mkono kikundi cha IS katika akaunti yake ya Facebook, waraka huo wa kiapo umeeleza.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG