Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:51

Harakati za kigaidi zabadilisha mbinu za mashambulizi Afrika-Wataalam


Kikundi cha kigaidi cha ISIS
Kikundi cha kigaidi cha ISIS

Juhudi za Marekani katika kupambana na ugaidi huko Afrika zinakabiliwa na matatizo mengi, pengine hakuna kati ya hayo matatizo yanayokera, au kuwa hatarishi, na kumeendelea kuwepo hali ya magaidi wenyewe kuvunja ushirikiano na kukiuka malengo yao.

Hivi sasa mafungamano sio kwa kikundi kimoja au itikadi moja, au wakati mwengine ni nani analipa zaidi. Hao wanaotekeleza operesheni za kigaidi wanaendelea kutokuwa wawazi na kukigawanya kikundi kimoja kutoka kingine.

Matokeo, kwa mujibu wa maafisa wa ulinzi na usalama wa nchi za Magharibi na Afrika, ni kuwepo kiwango cha juu cha aina mpya ya wanaoendesha ugaidi, ambao wako tayari kushirikiana na vikundi vya kigaidi vyenye ushindani mkubwa kama vile al-Qaida na Islamic State, na wakati mwengine wanatumikia pande zote.

“Unahitaji kuwa na teknolojia ambayo inaweza kufuatilia mabadiliko haya na utalazimika kutopitwa na matukio ili kufahamu ni kikundi gani cha wapiganaji hao wana mafugamano na kikundi kingine,” Christopher Maier, mkurugenzi wa kikosi cha kuitokomeza ISIS ameiambia VOA.

“Kimsingi wanaungana na kuwaingiza wapiganaji mara kwa mara,” amesema. “Uwezo wa wapiganaji hao na viongozi wao unatumika kadiri watavyoweza kukidhi maslahi yao katika eneo walilokuwepo.”

Matokeo yake, katika matukio ya mashambulizi ya kigaidi ni vigumu sana kutambua nani ameyafanya shambulizi, ambapo baadhi ya mashambulizi yakiwa ni mchango wa vikundi zaidi ya kimoja.

Kutambua mashambulizi kama hayo imepelekea kuhitalafiana kati ya taasisi za Marekani zinazopambana na ugaidi na maafisa wake.

XS
SM
MD
LG