Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:25

Marekani yaishambulia ISIS Somalia


African Command katika Pembe ya Afrika
African Command katika Pembe ya Afrika

Marekani imefanya shambulizi la anga kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya wapiganaji wa Kikundi cha Islamic State nchini Somalia Ijumaa na kusema imepiga hatua ya kipekee katika vita hii.

Katika miezi ya karibuni, Marekani imeendelea kushambulia wapiganaji jihadi kutoka katika kikundi cha waasi cha al-Shabaab ambacho kinamafungamano na al-Qaeda, lakini yaliyotokea Ijumaa ni hatua kubwa iliyofikiwa kutokana na kuendelea kwa vita hii dhidi ya IS.

“Majeshi ya Marekani yataendelea kutumia njia zote zinazokubalika na muwafaka kulinda Wamarekani na kuvidhoofisha vikundi vya kigaidi,” AFRICOM imesema.

Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kushambulia kikundi hicho katika nchi ya Pembe ya Afrika, Maafisa wamesema.

Shambulizi hilo limefanywa katika eneo la kaskazinimashariki mwa Somalia na kuuwa “magaidi kadhaa,” Kikosi cha jeshi la Marekani cha Africa Command kimeleza katika tamko lake.

Kwa mujibu wa VOA, ambayo imemtaja mwenyekiti wa mji wa Qandala katika eneo ambalo linajitawala lenyewe huko Puntland, makombora sita yalipiga kambi ya IS katika Kijiji cha Buqa, kilomita 60 upande huo.

“Wakazi wa eneo hilo na wafugaji walishtushwa na shambulizi hilo na kutoweka kutoka sehemu hiyo,” Jama Mohamed Qurshe ameiambia VOA.

Mashambulizi ya angani

Msemaji wa kikosi cha AFRICOM Luteni Kamanda Anthony Falvo amesema hakuna raia waliokuwa karibu na eneo hilo lililokuwa limeshambuliwa.

“Walipiga maeneo waliokusudia kuyashambulia,” alisema, na kueleza kuwa haya yalikuwa ni mashambulizi ya awali dhidi ya IS nchini Somalia.

Shambulizi la kwanza lilifanyika katikati ya usiku kwa saa za Somalia na shambulizi la pili kufuatia saa tano mchana.

IS imedai kufanya shambulizi la kujitoa muhanga ndani ya nchi ya Somalia mwezi Mei, na kuuwa watu wasiopungua watano na kuendeleza harakati zake katika eneo linalotawaliwa na al-Shabaab.

Wapiganaji hao wanaongozwa na Mhubiri wa zamani wa al-Shabaab Abdiqadir Mumin, ambaye alihama kutoka Al-Qaeda kwenda kujiunga na IS Octoba 2015 na kuitwa ni “gaidi la kimataifa” na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mwezi Agosti.

Mumin alizaliwa Puntland na kuishi Sweden kabla ya kurudi Uingereza miaka ya 2000, ambapo alipewa uraia wa Uingereza.

XS
SM
MD
LG