Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 16:48

Marekani yathibitisha shambulizi dhidi ya al-Qaida


Rmani ya Libya

Kwa kushirikiana na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Libya (GNA), majeshi ya Marekani yamefanya shambulizi la anga yakilenga eneo karibu na mji wa Ubari, Libya, Machi 24, 2018.

Tarifa ya kikosi maalumu cha Marekani -Africa Command imesema shambulizi hilo limewauwa magaidi wawili wa kikundi cha al-Qa’ida akiwemo Musa Abu Dawud, kiongozi wa ngazi ya juu wa kikundi hicho katika eneo la Maghreb (AQIM); sehemu ya kaskazini magharibi ya Afrika.

Dawud alitoa mafunzo kwa wanakikundi wapya wa AQIM ili kufanya mashambulizi mbalimbali katika eneo hilo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa alikuwa akitoa msaada nyeti sana ikiwa ni pamoja na taarifa mbalimbali za maeneo, fedha na silaha kwa kikundi cha AQIM na kuviwezesha vikundi vya kigaidi kuitishia na kuishambulia Marekani na maslahi ya nchi za Magharibi katika eneo hilo.

Africa Command ilitoa taarifa za shambulio hili Machi 24. Sasa kwa kuwa taarifa za operesheni hiyo na tathmini ya hasara iliosababishwa na shambulizi hilo zimekamilika na hivyo Africom inaweza hivi sasa kuthibitisha kuuwawa kwa Dawud.

Kwa wakati huu, tathmini inaonyesha hakuna raia yoyote waliouwawa katika shambulizi hilo.

Operesheni ya kupambana na ugaidi zinafanywa kwa mujibu wa sheria za Marekani na Kimataifa. Shambulizi hili lilifanyika kufuatia amri iliotolewa na Bunge la Marekani- Congress mwaka 2001 ikiidhinisha kutumika kwa jeshi lake na kwa kushirikiana na GNA, imeeleza taarifa hiyo.

Al-Qaida na vikundi vingine vya ugaidi, kama vile ISIS, vimetumia fursa ya kukosekana serikali nchini Libya na kutumia mwanya huo kuweka maficho yake ambapo magaidi hao wanahujumu, wanahamasisha, na kuongoza mashambulizi ya kigaidi; kutafuta na kurahisisha kuhamia kwa wapiganaji magaidi wa kigeni; kuchangisha na kuhamisha fedha kwa ajili ya kufanikisha operesheni zake.

Iwapo hatua hazitachukuliwa, vikundi hivi vinaweza kuleta maafa kwa raia na majeshi ya kulinda amani, na kupanga mashambulizi dhidi ya raia wa Marekani na maslahi ya washirika wa Marekani katika eneo hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG