Tangazo la Netanyahu kabla ya muda wa mwisho usiku wa manane, lilikuja baada ya mazungumzo magumu na washirika wake. Netanyahu anasema anatarajia kumaliza mikataba ya kushirikiana madaraka na washirika wake kufikia wiki ijayo.
Hata kama atafanikiwa, Netanyahu anakabiliwa na kibarua kigumu mbele yake. Ataongoza muungano unaotawaliwa na washirika wa mrengo wa kulia na wa-Orthodox ambao unaweza kuwatenganisha watu wengi wa Israel, kuzua mzozo na Wapalestina na kuiweka Israel kwenye mkondo wa mgongano na washirika wake wa karibu.
Netanyahu ambaye yeye mwenyewe anakabiliwa na kesi ya rushwa anataka kurejea ofisini baada ya kukaa mwaka mmoja na nusu uliopita kama kiongozi wa upinzani.
Akiza Yoel Ariel, mkazi wa ndani aeleza: “ Tuna matumaini makubwa kwa serikali mpya. Tuna matumaini kwamba serikali itakuwa ya mrengo wa kweli wa kulia ambayo itafanya mengi mazuri kwa watu wa Israel, kwa taifa la Israel, kujenga nchi na kujenga makazi mapya.
Naye Eli Ram, mkazi wa ndani anasema: “ hii ni serikali mbaya, mbaya sana, serikali ya kibaguzi, na siiamini itadumu kwa zaidi ya mwaka mmoja nina matumaini kwamba haitafanikiwa.”