Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 11:35

Netanyahu kushirikiana na Ben-Gvir aliyewahi kuhusishwa na ugaidi kuunda serikali


Kiongozi wa chama cha Likud Benjamin Netanyahu akipunga mkono kwa wafuasi nje ya makao makuu ya chama chake mjini Jerusalem. Nov 2, 2022
Kiongozi wa chama cha Likud Benjamin Netanyahu akipunga mkono kwa wafuasi nje ya makao makuu ya chama chake mjini Jerusalem. Nov 2, 2022

Wapiga kura nchini Isreal wana hisia mbalimbali kufuatia taarifa za Benjamin Netanyahu kurejea madarakani kama waziri mkuu wa nchi hiyo.

Baada ya kura zote kuhesabiwa kufuatia uchaguzi wa jana matokeo ya awali yanaonesha kwamba Netanyahu, mwenye siasa za mrengo wa kulia, anaelekea kupata ushindi mkubwa.

Yossi Zarifi, ni muuzaji wa kahawa na mfuasi wa Netanyahu mjini Jerusalem.

" Ben-Gvir ndiye ameshitua watu katika uchaguzi huu. Alitarajiwa kupata umaarufu lakini sio kupata idadi ya wabunge ambao amepata. Nina matumaini kwamba serikali ya mrengo wa kulia itaunda serikali. Nina matumaini ya kupatikana kwa Israel yenye usimamizi wa wastan namna ilivyokuwa wakati wa utawala wa Arik. "

Uchaguzi huo uliofanyika Jumanne ni wa tano ndani ya kipindi cha chini ya miaka minne nchini Israel.

Taifa hilo linaangazia zaidi uwezo wa Netanyahu kuongoza serikali.

Anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi na utumiaji mbaya madaraka, lakini amekana mashtaka yote dhidi yake, na wafuasi wake wanahisi kwamba mashtaka hayo yamechochewa kisiasa, huku wapinzani wake wakimuona kama tisho kubwa kwa demokrasia ya Isreal.

Lakini ushirikiano wake na Ben Gvir kuunda serikali umetiliwa mashaka na wachambuzi pamoja na washirika wa Isreal. Ben Gvir alikuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Kach. Aliwahi pia kuhukumiw agerezani kwa makosa ya uchochezi.

Hata iwapo Netanyahu na washirika wake wataibuka washindi, itachukua wiki kadhaa za majadiliano ya kuunda serikali.

XS
SM
MD
LG