Tamko hilo limetolea licha ya wasi wasi kutoka kwa utawala wa Biden kuhusu viongozi atakaowachagua kwenye serikali yake yenye msimamo wa mrengo wa kulia.
Wakati akizungumza na kundi lenye msimamo wa mrengo wa kushoto ambalo linalaumiwa kuwaunga mkono wapalestina pamoja na Iran, Blinken amesema kwamba Marekani itabaki kuwa rafiki wa karibu wa Israel.
Hilo litafanyika licha ya kuwa na misimamo tofauti na Ntenyahu kama vile kuundwa kwa mataifa mawili katika kutatua mzozo kati ya Israel na Palestina, pamoja na kurejeshwa kwa mkataba wa nyuklia wa Iran wa 2015.
Ameongeza kusema kwamba ushirikiano uliopo kati ya Marekani na Israel ni thabiti kuliko wakati wowote ule.