Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 03:49

Waziri mkuu wa Israel kuivunja serikali na kuitisha uchaguzi mpya


Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennett akihudhuria mkutano wa baraza la mawaziri mjini Jerusalem, May 15, 2022. Picha ya Reuters

Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Naftali Bennett imetangaza kwamba serikali ya muungano ya nchi hiyo itavunjwa, na hivyo uchaguzi mwingine kuandaliwa.

Bennett na mshirika wake mkuu, Yair Lapid, watalivunja bunge katika siku zijazo, ofisi ya Bennett imesema. Lapid atahudumu kama waziri mkuu wa mpito hadi serikali mpya itakapoundwa.

Serikali ya Bennett ilikuwa dhaifu tangu ilipoingia madarakani mwaka mmoja uliopita, muungano wa vyama vinane tofauti unaojumuisha vyama vya mrengo wa kulia, vya kiliberali na vyama vya Waarabu Waislamu.

Muungano huo ulianza kugawanyika baada ya maafisa kadhaa wa chama cha Bennett kujiondoa kwenye muungano huo, wakisema wanahisi kwamba Bennett anakubaliana maelewano mengi na washirika wake.

Uchaguzi mpya utampa fursa waziri mkuu wa zamani wa muda mrefu Benjamin Netanyahu ya kurudi madarakani.

Netanyahu hivi sasa ni kiongozi wa upinzani baada ya kukaa madarakani kwa miaka 12.

Siku ya Ijumaa alisema kuvunjwa kwa bunge "itakuwa habari njema" kwa mamilioni ya Waisraeli na kutabiri kwamba chama chake cha Likud kitaongoza serikali mpya.

Bennett aliunda serikali ya muungano wa vyama vinane mwaka jana baada ya chaguzi nne mfululizo ambazo hazikubaini mshindi.

Uchaguzi ujao utakuwa wa tano kwa Israel katika kipindi cha miaka mitatu.

Waziri wa ulinzi Benny Gantz amesema kwenye Twitter Jumatatu kwamba serikali itaendelea na shughuli zake, hata wakati wa kipindi cha mpito.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG