Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:28

Wahamiaji 28 wakutikana wamekufa Pwani ya Libya


Wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakisubiri msaada wakiwa katika boti ya mbao iliyokuwa imesheheni katika Bahari ya Mediterranean maili 122 nje ya pwani ya Libya Feb. 12, 2021. (AP Photo/Bruno Thevenin)
Wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakisubiri msaada wakiwa katika boti ya mbao iliyokuwa imesheheni katika Bahari ya Mediterranean maili 122 nje ya pwani ya Libya Feb. 12, 2021. (AP Photo/Bruno Thevenin)

Miili ya wahamiaji 28 imesukumwa na maji kwenye pwani ya magharibi mwa Libya baada ya boti yao kuzama, afisa wa usalama amesema Jumapili, ikiwa ni maafa mapya katika njia yenye maafa makubwa ambayo hutumiwa na wahamiaji.

“Timu ya Shirika la Mwezi Mwekundu la Libya limepata miili 28 ya wahamiaji waliofariki na kuwapata manusura watatu katika maeneo mawili tofauti katika fukwe za Al-Alous,” takriban kilomita 90 kutoka Tripoli, vyanzo vya habari vimeeleza.

“Miili hiyo ilikuwa katika hatua za awali za kuharibika imeashiria kwamba ajali ya meli ilitokea siku kadhaa zilizopita,” amesema, akiongeza kuwa idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka katika saa kadhaa zijazo.

Picha zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari vya Libya zimeonyesha maiti zilizopangwa katika ufukwe na kisha kuwekwa katika mifuko.

Libya, iliyogubikwa na muongo mzima vita na ukosefu wa sheria, imekuwa ni sehemu kuu ya safari za wahamiaji wa kiafrika na kutoka Asia wanaofanya majaribio ya kukata tamaa kufika Ulaya.

Wahamiaji mara nyingi wanavumilia hali mbaya iliyoko nchini Libya kabla ya kuanza kuelekea nchi za kaskazini katika vyombo vya baharini vyenye msongamano mkubwa na visivyokuwa salama ambavyo mara kwa mara huzama au kupata matatizo.

Maafa haya ya hivi karibuni yametokea siku kadhaa baada ya wahamiaji 160 kufariki ndani ya wiki moja katika matukio kama hayo, ikifanya idadi ya waliopoteza maisha mwaka 2021 kufikia 1,500, kulingana na Jumuiya ya Kimataifa inayofuatilia Wahamiaji.

IOM imesema zaidi ya wahamiaji 30,000 wamekamatwa katika kipindi hicho na kurejeshwa Libya.

Umoja wa Ulaya umeshirikiana kwa karibu na Walinzi wa Pwani wa Libya kupunguza idadi ya wahamiaji wanaowasili katika pwani za Ulaya.

Wanaporejea huko, wengi hukabiliwa na manyanyaso zaidi kutisha katika vituo vinavyowashikilia.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG