Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 16:26

Baadhi ya wapiganaji wa kigeni waondoka Libya


Baadhi wa wapiganaji mjini Tripoli kwenye picha ya zamani
Baadhi wa wapiganaji mjini Tripoli kwenye picha ya zamani

Waziri wa mambo ya nje wa Libya,Jumapili amesema baadhi ya wapiganaji wa kigeni wameondoka nchini humo, wakati serikali ya umoja ikitafuta msaada wa kimataifa kuwaondoa wengine wengi waliobaki.

“ Ripoti hizi ni sahihi. Ni mwanzo mzuri”, waziri Najla Mangoush amesema kwenye mkutano wa waandishi wa habari nchini Kuwait alipoulizwa iwapo baadhi ya wapiganaji wa kigeni walifukuzwa.“Bado tunaanda mipango makubwa na ya kina ili kuwaondoa mamluki”, amesema.

Hakuna hatua kubwa za kuwaondoa mamluki wa kigeni zilizofanyika kutokana na maelezo juu ya mchango wa majeshi ya kikanda yanayoshirikiana na kila upande na kukwamisha juhudi za kuafikiana juu ya kanuni za msingi za uchaguzi wa kitaifa.

Hakujapatikana amani au usalama wa kutosha nchini Libya tangu mwaka 2011 wakati majeshi ya muungano wa NATO yaliposaidia katika kumuondoa madarakani rais Muammar Gaddafi. Nchi iligawanyika kati ya makundi ya mashariki na magharibi yaliyopigana mwaka 2014.

Jeshi la mashariki liliungwa mkono na Umoja wa falme za kiarabu, Russia na Misri. Serikali ya awali ya mjini Tripoli iliyopo upande wa magharibi ilitambuliwa na Umoja wa mataifa na kuungwa mkono na Uturuki.

Pande zinazopigana zilileta mamluki, ikiwemo kutoka kundi la Wagner la Russia, Syria, Sudan na Chad kati ya nchi nyingine, Umoja wa mataifa umesema.

XS
SM
MD
LG