Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 02:20

Watu wenye bunduki washambulia mahakama Libya wakati Gaddafi anaasilisha rufaa


Ofisi ya Umoja wa mataifa nchini Libya, UNSMIL leo imelani shambulio dhidi ya mahakama ya mji wa Sebha, ambayo ilipinga Seif al Islam Kadhafi asikate rufaa dhidi ya uamzi wa kumkatalia kugombea urais kwenye uchaguzi unaopangwa kufanyika tarehe 24 Disemba mwaka huu.

Alhamisi jioni, watu wenye silaha wasiojulikana waliingia ndani ya mahakama ya Sebha ambayo inapokea rufaa za wagombea urais, na kuilazimisha kusitisha shughuli zake, wakati mawakili wa mtoto huyo wa rais wa zamani Moummar Kadhafi wakijianda kuwasilisha rufaa dhidi ya uamzi wa kupinga kugombea kwa Seif al Islam.

Ofisi hiyo ya Umoja wa mataifa ambayo imesema kushtushwa na shambulio hilo, imelani vurugu za aina yoyote zinazohusiana na uchaguzi, na kutoa wito mwengine wa kulinda mchakato wa uchaguzi.

Taarifa ya UNSMIL imeongeza kuwa “ mashambulizi dhidi ya vifaa vya mahakama na uchaguzi sio tu vitendo vya uhalifu ambavyo vinaadhibiwa na sheria ya Libya, lakini pia vinahujumu haki ya Walybia ya kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi”.

Serikali ya mpito ya Libya jana ililani kitendo hicho kibaya na kutangaza kwamba uchunguzi umeanzishwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG