Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:55

Wahamiaji wafa maji kwenye ufukwe wa Libya


Wahamiaji waliookolewa karibu na ufukwe wa Libya katika video ya awali
Wahamiaji waliookolewa karibu na ufukwe wa Libya katika video ya awali

Watu 57 wamekufa maji Jumatatu baada ya boti yao kupinduka kwenye pwani ya Libya karibu na Khums, ukiwa msiba mkubwa sana kutokea hivi karibuni katika eneo la kati la Mideterania, shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji(IOM) limesema.

“Kulingana na manusura waliofikishwa ufukweni na wavuvi na walinzi wa pwani, wanawake ishirini na watoto wawili ni miongoni mwa waliokufa maji”, msemaji wa IOM, Safa Msehli amesema kwenye twitter.

Boti za wahamiaji wanaosafiri kuelekea Italy na maeneo ya Ulaya wakitokea Libya na Tunisia, zimeongezeka miezi ya karibuni kutokana na hali nzuri ya hewa.

Maelfu ya wahamiaji wamefanya safari hatari ya kuvuka bahari miaka iliyopita, wakikimbia mizozo na umaskini barani Afrika na mashariki ya kati.

XS
SM
MD
LG