Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:41

Wahamiaji 17 wazama Bahari ya Mediterranean


FILE - Wahamiaji wakisubiri kuokolewa na shirika la Ocean Viking wakati wa operesheni ya utafutaji na ukoaji katika Bahari ya Mediterranean Julai 5, 2021. (Flavio Gasperini/SOS Mediterranee/Handout via Reuters)
FILE - Wahamiaji wakisubiri kuokolewa na shirika la Ocean Viking wakati wa operesheni ya utafutaji na ukoaji katika Bahari ya Mediterranean Julai 5, 2021. (Flavio Gasperini/SOS Mediterranee/Handout via Reuters)

Wahamiaji wasiopungua 17 raia wa Bangladesh walizama kwenye boti iliyopasuka na kuzama kwenye pwani ya Tunisia wakati wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterranean kwenda Italia kutoka Libya.

Katika ajali hiyo watu wengine zaidi ya 380 waliokolewa na walinzi wa pwani, Kituo cha Shirika la Mwezi Mwekundu cha Tunisia kimeeleza Jumatano.

Boti hiyo ilikuwa imeanza safari kutoka Zuwara, pwani ya kaskazini magharibi mwa Libya, ikiwa imewabeba wahamiaji kutoka Syria, Misri, Sudan, Eritrea, Mali na Bangladesh, taasisi hiyo ya misaada ya kibinadamu ilieleza.

Wabengali 17 walifariki dunia na wahamiaji zaidi ya 380 waliokolewa katika mashua iliyokuwa ikitoka Zuwara ya Libya kuelekea Ulaya, afisa wa mwezi mwekundu Mongi Slim alisema.

Katika miezi ya hivi karibuni, watu kadhaa wamezama kwenye pwani ya Tunisia, na kuna ongezeko la mzunguko wa majaribio ya kuvuka kwenda Ulaya kutoka Tunisia na Libya kuelekea Italia wakati hali ya hewa ikiwa imeimarika.

Chanzo cha Habari : Reuters

XS
SM
MD
LG