Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:10

Wafuasi wa Rais wa Tunisia wajitokeza kuunga mkono kusimamishwa bunge


Maandamano kumunga mkono rais wa Tunisia Kais Saied.(Photo by Fethi Belaid / AFP)
Maandamano kumunga mkono rais wa Tunisia Kais Saied.(Photo by Fethi Belaid / AFP)

Maelfu ya wafuasi wa Rais wa Tunisia Kais Saied walikusanyika katika mji mkuu Jumapili kuonyesha uungaji mkono kwa hatua yake ya kulisimamisha bunge na ahadi zake za kubadilisha mfumo wa kisiasa, kitendo ambacho wakosoaji wake wanakiita ni mapinduzi.

Mandamnao katikati ya Tunis yaliitishwa kujibu maandamano yaliyofanyika mara mbili mwishoni mwa wiki siku za nyuma katika eneo hilo hilo kupinga hatua za Saied. Inatarajiwa maadamano ya leo kuwa na idadi kubwa zaidi ya maandamano yaliyotangulia.

Waandamanaji walipeperusha bendera za Tunisia na kubeba mabango wakipinga Ennahda, chama cha Islamist chenye msimamo wa wastani ambacho ndio kina viti vingi katika bunge na kimekuwa kikisimama kama mpinzani mkuu wa Saied.

“Tunamtaka rais alivunje bunge na kuwawajibisha wale waliosababisha watu kutaabika kwa muongo moja,” Salem Ajoudi, mmoja wa waandamanaji alisema.

Rais aliitumbukiza Tunisia katika mgogoro wa kikatiba mwezi Julai kwa kusitisha bunge lililokuwa limechaguliwa, kumfukuza waziri mkuu na kutumia amri za kiutendaji.

Mwezi uliopita alipuuza sehemu kubwa ya katiba kwa kusema anaweza kupitisha sheria kwa kutumia amri ya kiutendaji, na kuweka shaka kwa mafanikio ya kidemokrasia ya Tunisia yaliyopatikana wakati wa mapinduzi ya 2011 yaliyosababisha ghasia za “Arab Spring” kote katika dunia ya Kiarabu.

Uingiliaji kati wa Saied unafuatia miaka ya kukwama kiuchumi na kukwama kisiasa kulikoongezeka kutokana na masharti yaliyowekwa ya kutotoka nje katika taifa hilo maskini mwaka jana, kususua kwa kuanza kwa kampeni ya chanjo na maandamano ya mitaa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG