Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:27

Tunisia yapata medali ya kwanza ya dhahabu katika Olimpiki


Muogeleaji wa Tunisia Ahmed Hafnaoui ameushangaza ulimwengu baada ya kutwaa medali ya dhahadu katika mita 400 wanaume Tokyo Japan.
Muogeleaji wa Tunisia Ahmed Hafnaoui ameushangaza ulimwengu baada ya kutwaa medali ya dhahadu katika mita 400 wanaume Tokyo Japan.

Hatimaye bara la Afrika limetoka kimaso maso katika michuano ya Olimpiki kwa upande wa kuogelea baada ya Muogeleaji Ahmed Hafnaoui wa Tunisia kuwa Mwafrika wa kwanza kubeba medali ya dhahabu kwenye michuano hiyo alipomaliza katika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanaume mita 400 siku ya Jumapili.

Muogeleaji huyo mwenye umri wa miaka 18 aliushangaza ulimwengu baada ya kumuacha raia wa Australia Jack McLoughin ambaye alikuja sekunde 16 nyuma yake na kuchukua nafasi ya pili mapema wakati Mmarekani Kieren Smith alipata medali ya shaba.

Ilikuwa medali ya pili kwa Tunisia huko Tokyo baada ya Mohamed Khalil Jendoubi kushinda medali ya fedha katika taekwondo ya wanaume ya kilo 58.

XS
SM
MD
LG