Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 20:58

Wananchi wengi wa Tunisia wafurahia kuteuliwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke


Rais Kais Saied wa Tunisia akutana ofisini mwake waziri mkuu mpya Najila Bouden Romdhane
Rais Kais Saied wa Tunisia akutana ofisini mwake waziri mkuu mpya Najila Bouden Romdhane

Wananchi wengi wa Tunisia waeleza furaha zao baada ya Rais Kais Saied kumteua Najla Bouden, mwanajiolojia kua mwanamke wa kwanza waziri mkuu wa Tunisia na halikadhalika wa kwanza katika nchi za Kiarabu.

Dk. Bouden, profesa asiyejulikana sana katika siasa za Tunisia, ni mtaalamu wa jiolojia ambaye alitekeleza miradi ya Benki Kuuya Dunia katika wizara ya elimu, kuimarisha mfumo wa masomo ya juu.

Rais Saied alichukua uwamuzi huo Jumatano, akiwa anakabiliwa na shinikizo la ndani na la kimataifa kumtaka kutaja serikali baada ya kumfukuza kazi waziri mkuu Hichem Mechichi, kusimamisha bunge na kuchukua mamlaka ya uongozi Julai 25, hatua ambayo wapinzani wake wamezieleza kua ni mapinduzi.

Ofisi ya Saied ilichapisha video akikutana na waziri mkuu mpya Ramadhane ofisini kwake na kumpa, mamlaka ya kupendekeza baraza la mawaziri katika muda mfumo ujao.

"Kazi lazima ifanyike haraka na timu ambayo utaongoza lazima iwe na mchanganyiko wa watu wote na ifanye kazi kwanza kabisa katika kupambana na ufisadi," amesema Saied

Wakati wa mkutano huo alisisitiza mara kwa mara kwamba ni jambo la kihistoria kuteuliwa kwa mwanamke katika nafasi hiyo, akisema ni heshima kwa Tunisia na heshima kwa wanawake wa taifa hilo.

Rais Kais Saied wa Tunisia amkaribisha ofisini mwake waziri mkuu mteule Najila Bouden Romdhane
Rais Kais Saied wa Tunisia amkaribisha ofisini mwake waziri mkuu mteule Najila Bouden Romdhane

Saied alisema dhamira kuu ya serikali mpya itakuwa kumaliza ufisadi na ukosefu wa nidhamu hali iliyoenea katika taasisi nyingi za serikali.

"Tutafanya kazi pamoja katika siku za usoni na dhamira thabiti ya kuondoa ufisadi na machafuko yaliyoenea katika taasisi nyingi za serikali." amesema rais Saied

Bouden atakuwa waziri mkuu wa kumi wa Tunisia tangu ghasia za mwaka 2011 zilizompindua dikteta wa muda mrefu Zine El Abedine Ben Ali, na kusababisha mapinduzi ya nchi za Kiarabu.

Nchi hiyo imesifiwa kimataifa kwa mabadiliko yake ya kidemokrasia lakini watu wengi wa Tunisia wanasema hawajaona mabadiliko makubwa katika maisha yao na wamekatishwa tamaa na mchakato usiofaa wa kisiasa na ufisadi.

Hatua za Saied zina mpatia madaraka makubwa ya kiutendaji, ambayo yeye mwenyewe ataongoza baraza la mawaziri.

Najla Bouden, mwenye umri sawa na Saied wa miaka 63, ni mkurugenzi wa zamani wa mradi wa mageuzi ya elimu ya juu, na ameshikilia nyadhifa za juu katika wizara ya elimu ya juu ya Tunisia.

waaziri mkuu mpya anatokea Kairouan, mji wa kaskazini mwa Tunisia, na ni mtaalam wa jiolojia aliyesomea Ufaransa akiwa shahada ya usamivu wa uhandisi wa jiolojia, na ni mhadhiri katika shule ya uhandisi ya kitaifa ya Tunisia.

XS
SM
MD
LG