Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:43

Wabunge wa Kimataifa wanaounga mkono vikwazo dhidi ya China wakutana Washington


Balozi wa Taiwan nchini Marekani Hsiao Bi-khim.
Balozi wa Taiwan nchini Marekani Hsiao Bi-khim.

Balozi  wa Taiwan mjini Washington, Hsiao Bi-khim, siku ya Jumanne alikuwa mwenyeji wa darzeni ya wabunge wa kimataifa ambao wanaunga mkono vikwazo dhidi ya China.

Wabunge hao wanaunga mkono vikwazo hivyo kutokana na vitendo vya China vya uchokozi kwa kisiwa hicho, ikiwa ni ishara ya kuiunga mkono Taipei katikati ya shinikizo la kijeshi linalofanywa na Beijing.

Mkusanyiko huo ambao haukutangazwa wa wabunge takriban 60 kutoka Ulaya, Asia na Afrika katika jengo la ubalozi wa Taiwan lilioko kilimani Washington – linaloitwa Twin Oaks – ni hatua ya karibuni katika juhudi za serikali ya Taipei kuzishawishi demokrasia nyingine rafiki kusimama dhidi ya China tangu uvamizi wa Russia nchini Ukraine ulivyoongeza wasiwasi kuwa Beijing inaweza kujaribu kukichukua kisiwa hicho kwa nguvu.

Ubalozi wa Taiwan mjini Washington DC.
Ubalozi wa Taiwan mjini Washington DC.

Kikundi hicho, ambacho kina wanachama wa Umoja wa Wabunge maarufu Inter-Parliamentary Alliance on China (IPAC) kilikusanyika Washington wiki hii, na kutarajiwa kusaini ahadi yao kuzishinikiza serikali zao kuchukua msimamo “ kupigania kuzuia zaidi hatua za kijeshi au shinikizo jingine lolote” za harakati za Jamhuri ya Watu wa China (PRC) dhidi ya Taiwan, kulingana na rasimu ambayo Reuters iliiona.

Imeongeza kuwa mahusiano kati ya nchi zao na Taiwan siyo juu ya Beijing kuamua yawepo, na watashinikiza kuongeza idadi ya ziara za uhusiano mwema zinazofanywa na wabunge wa nchi zao.

“Tutaendelea kufanya kampeni kuhakikisha serikali zetu zinapeleka ujumbe kwa PRC kuwa uchokozi wowote wa kijeshi dhidi ya Taiwan utaigharimu Beijing thamani kubwa. Hatua za kiuchumi na kisiasa, ikiwemo vikwazo vikali, vitafikiriwa ili kuzuia hatari za kijeshi, na kuhakikisha biashara na aina nyingine ya mabadilishano na Taiwan yanaendelea bila kizuizi,” rasimu hiyo imeeleza.

Wamarekani wenye asili ya Taiwan wakiwa mbele ya ubalozi wa China mjini Washington, DC kupinga mazoezi ya kijeshi yakitumia silaha za moto yanayoendeshwa na China kuzunguka nchi ya Taiwan baada ya Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi kufanya ziara katika visiwa hivyo. August 12. 2022.
Wamarekani wenye asili ya Taiwan wakiwa mbele ya ubalozi wa China mjini Washington, DC kupinga mazoezi ya kijeshi yakitumia silaha za moto yanayoendeshwa na China kuzunguka nchi ya Taiwan baada ya Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi kufanya ziara katika visiwa hivyo. August 12. 2022.

Rais wa China Xi Jinping ameahidi kuileta Taiwan inayotawaliwa kidemokrasia chini ya himaya ya Beijing na hajafuta uwezekano wa kutumia nguvu. Amejiandaa kuwania awamu ya tatu, ya uongozi wa kipindi cha miaka mitano katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Kikomunisti mwezi ujao. Serikali ya Taiwan inakanusha vikali madai ya China kuitawala Taiwan.

FILE - Rais Vladimir Putin, kulia, na Rais Xi Jinping wakiingia kufanya mazungumzo Kremlin, Moscow, Russia, June 5, 2019.
FILE - Rais Vladimir Putin, kulia, na Rais Xi Jinping wakiingia kufanya mazungumzo Kremlin, Moscow, Russia, June 5, 2019.

Vyanzo vya habari vinavyojua suala hili vimeiambia Reuters kuwa Washington inatathmini vikwazo dhidi ya China kuizuia kuivamia Taiwan, huku Umoja wa Ulaya ukiwa chini ya shinikizo la kidiplomasia kutoka Taipei kuchukua hatua sawa na hiyo.

Hsiao, akizungumza na wabunge – ambao kulingana na orodha ya wageni iliyowafikia Reuters wanatoka nchi zikiwemo Uingereza, Australia, Canada, India, Japan, Lithuania, Ukraine, New Zealand na Holland – ameuambia mkusanyiko huo: “Ni muhimu kumuonyesha mbabe huyo kwamba sisi tunao marafiki pia.

“Sisi hatutafuti kumchokoza mbabe huyo, lakini pia hatuwezi kusalimu amri kwa shinikizo lao.”

Aliwakaribisha wawakilishi wawili wa Ukraine katika tukio hilo.

“Kwa hakika ni matumaini yetu kuwa wakati jumuiya ya kimataifa inasimama na Ukraine, jumuiya hiyo ya kimataifa pia itasimama na Taiwan… kwa pamoja tunaweza kuzuia uchokozi zaidi unaoletwa na China usitokee.”

Wabunge kutoka darzeni ya nchi wakiwa pamoja na wanaharakati wa Hong Kong, Tibet, Xinjiang walipokutana Rome wakati mkutano wa G20 ukifanyika Octoba 2021.
Wabunge kutoka darzeni ya nchi wakiwa pamoja na wanaharakati wa Hong Kong, Tibet, Xinjiang walipokutana Rome wakati mkutano wa G20 ukifanyika Octoba 2021.

Ahadi ya IPAC, inayotarajiwa kusainiwa Jumatano, pia inatoa wito kwa nchi mbalimbali kudhibiti usambazaji bidhaa unaotokana na watu kulazimishwa kufanya kazi katika mkoa wa Xinjiang nchini China, na kuweka vikwazo kwa maafisa wa China kutokana na manyanyaso wanayofanya Hong Kong, na kwa makampuni ya Kichina ambayo yanasaidia viwanda vya kijeshi Russia.

Ubalozi wa China mjini Washington haukujibu ombi la kueleza maoni yao kuhusu madai hayo.

XS
SM
MD
LG