Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:17

China imeendelea kufyatua makombora katika bahari karibu na Taiwan


Ndege za kivita ya jeshi la China ikipaa katika bahari ya Taiwan karibu na Pingtan. Aug 5 2022. Picha: AP
Ndege za kivita ya jeshi la China ikipaa katika bahari ya Taiwan karibu na Pingtan. Aug 5 2022. Picha: AP

Jeshi la China limetangaza kuendelea na mazoezi ya kijeshi katika bahari karibu na mpaka na Taiwan, siku moja baada ya kumalizika kwa muda uliokuwa umetangazwa awali.

Mazoezi hayo ya kijeshi ni makubwa zaidi kuwahi kufanywa na China, wakilalamikia ziara ya spika wa baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi nchini Taiwan.

China imesema kwamba mazoezi yake yataangazia zaidi operesheni ya kijeshi baharini, na hatua hiyo imepelekea hofu kwamba huenda Beijing itaendelea kushinikiza kutaka kuuchukua utawala wa Taiwan.

Wizara ya mambo ya nje ya Taiwan imeikosoa hatua hiyo ya China, ikisema kwamba ilikuwa inasababisha mgogoro makusudi, na kutaka kuacha mazoezi hayo.

XS
SM
MD
LG