Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:52

China yapiga marufuku uagizaji bidhaa kutoka Taiwan


Soko la matunda mjini Taipei, Taiwan.
Soko la matunda mjini Taipei, Taiwan.

China Jumatano imepiga marufuku uagizaji wa matunda na samaki kutoka Taiwan wakati pia ikisitisha upelekaji wa mchanga wa ujenzi kisiwani humo, kufuatia ziara iliyozua utata ya spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi.

Ziara ya Pelosi ya Taiwan Jumanne jioni ni ya kwanza ya afisa wa ngazi ya juu wa Marekani baada ya miaka 25, na imezua mvutano mkubwa wa kidiplomasia kati ya China na Marekani, kwa kuwa China inadai kumiliki kisiwa hicho kinachojitawala. Pelosi alitua Taiwan licha ya onyo la awali kutoka China la kutofanya hivyo.

Wakati huo huo serikali ya China imetangaza mpango wa mazoezi ya kijeshi yenye silaha za moto kuzunguka Taiwan, hatua ambayo imetajwa na wizara ya ulinzi ya Taiwan kama tishio la bandari zake pamoja na miji muhimu.

Kumekuwa na ongezeko la mivutano kati ya China na Taiwan tangu rais Tsai Ing-WEN kuchukua madaraka mwaka wa 2016 akidai kwamba kisiwa hicho ni taifa linalojitawala na wala siyo sehemu ya China. Wakazi milioni 23 wa Taiwan kwa muda mrefu wameishi kwa hofu ya kushambuliwa na China lakini hofu hiyo imeongezeka zaidi wakati wa utawala wa rais Xi Jingping wa China.

XS
SM
MD
LG