Upatikanaji viungo

Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 20:57

Wabunge 73 wachaguliwa katika uchaguzi unaoendelea Somalia


FILE - Bunge la Somalia wakipiga kura kwa kunyoosha mikono, Mogadishu, Somalia, Sept. 23, 2020.

Tume ya uchaguzi nchini Somalia inasema wabunge 73 kati ya 275 wamechaguliwa kufikia sasa.

Uchaguzi usio wa moja kwa moja unaendelea katika majimbo ya wabunge kadhaa nchini humo.

Uchaguzi huo ulianza mwezi Novemba na ulikuwa umepangwa kumalizika Desemba 24 lakini mchakato umecheleweshwa kutokana na tofauti zilizojitokeza.

Waziri mkuu Mohamed Hussein Robe, na viongozi wa majimbo walifikia makubaliano Januari 9, kuhakikisha kwamba uchaguzi huo unakamilia Februari 25.

Mchakato huo mpana, unawahusisha viongozi wa kijamii kuwachagua wawakilishi, ambao huchagua wabunge.

Maseneta, huchaguliwa na mabunge ya majimbo.

Kikao cha Pamoja cha mabaraza mawili ya bunge humchagua rais. Tarehe ya kumchagua rais haijatangazwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG