Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:40

Al-Shabaab wameshambulia mji huko Mogadishu na kuwaua askari na raia


Picha za kundi la Al-Shabaab la nchini Somalia
Picha za kundi la Al-Shabaab la nchini Somalia

Polisi na wakaazi wa Balad mji uliopo kiasi cha kilomita 30 kaskazini mwa Mogadishu walisema wapiganaji wa kundi lenye uhusiano na al-Qaida walishambulia na kuvamia vikosi vya serikali vinavyolinda daraja kwenye lango la mji huo mapema asubuhi

Wapiganaji wa kundi la al-Shabaab la Somalia waliushambulia mji kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu leo Alhamis na kuua takribani watu saba wakati wakipambana na vikosi vya usalama vya serikali, afisa wa polisi na wakaazi walisema.

Polisi na wakaazi wa Balad mji uliopo kiasi cha kilomita 30 kaskazini mwa Mogadishu walisema wapiganaji wa kundi lenye uhusiano na al-Qaida walishambulia na kuvamia vikosi vya serikali vinavyolinda daraja kwenye lango la mji huo mapema asubuhi. "Tulikuwa msikitini tukiswali wakati wa mapambano makali ya risasi yalipotokea kwenye daraja hilo". Al- Shabaab waliuteka mji huo na kuwapita wanajeshi kwenye daraja Hassan Nur, muuza duka mjini Balad mji wa kilimo unaunganisha mkoa wa Middle Shabelle na Lower Shabelle nchini Somalia, aliliambia shirika la habari la Reuters.

Kulikuwa na vikosi vichache vya polisi mjini humo. Polisi walipotea, wakati ufyatuaji risasi ulipoanza na watu walikimbia kwenye nyumba zao. Nilihesabu wanajeshi watano walikufa na raia wawili wanawake, alisema.

XS
SM
MD
LG