Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:39

Bunge la Uingereza kujadili Uhuru wa Somaliland


Bunge la Uingereza..
Bunge la Uingereza..

Bunge la Uingereza linatarajiwa kujadili hoja iliyopewa kichwa cha Habari “ kuitambua Somaliland” ambayo imewasilishwa na mbunge Gavin Williamson.

Somaliland ilijitenga na somalia zaidi ya miaka 30 iliyopita lakini haitambuliwi kama taifa huru na umoja wa Africa au umoja wa mataifa.

Wizara ya mambo ya nje ya Somaliland imekaribisha hoja hiyo na kutoa wito kwa wakazi wake nchini Uingereza kuwasiliana na wabunge wao kuhusu suala hilo.

Serikali za mitaa za Uingereza katika miji ya Sheffield, Cardiff na Birmingham zinaunga mkono uhuru wa Somaliland, lakini serikali ya Uingereza haiungi mkono.

XS
SM
MD
LG