Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:11

Waandamanaji wapinga 'lockdown' na masharti mengine Kenya


Vijana bawili wanauza njugu mbele ya tangazo linalowashauri watu kuchukua tahadhari dhidi kupata maambukizi mapya ya virusi vya corona, katika eneo la Kibera ambalo ni makazi ya watu yasiorasimishwa, Nairobi, Kenya, Alhamisi, Aprili 2, 2020.
Vijana bawili wanauza njugu mbele ya tangazo linalowashauri watu kuchukua tahadhari dhidi kupata maambukizi mapya ya virusi vya corona, katika eneo la Kibera ambalo ni makazi ya watu yasiorasimishwa, Nairobi, Kenya, Alhamisi, Aprili 2, 2020.

Darzeni za waandamanaji wenye ghadhabu wamepambana na polisi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumatano, wakitaka amri ya kutotoka nje iondolewe.

Pia wanashinikiza kusitishwa kwa masharti mengine yaliyowekwa na serikali, ili kupambana na kuenea kwa virusi vya Corona.

Kadhalika waandamanaji hao walitaka kumalizika kwa kile wanachokiita "ukatili wa polisi" katika taifa hilo la Afrika Mashariki, haswa dhidi ya vijana.

Polisi waliwatawanya waandamanaji hao kwa kufyatua risasi hewani, kurusha gesi ya machozi, na kuwakamata watu kadhaa.

Jane Atieno ambaye ni kati ya waandamanaji hao anasimulia hali ilivyokuwa : "Tuko hapa kuzungumza juu ya vijana wetu jinsi walivyouawa, jinsi wanavyoteseka. Tunataka haki zetu. Vijana wetu hawana kazi, vijana wetu wanauawa, Vijana wetu wanateseka ; wameugua kwa sababu ya ukosefu wa kazi; kwa sababu ya kukosa kila kitu. Tunaiuliza nchi yetu; tunamuomba Rais wetu awasaidie vijana wetu. "

Serikali ya Kenya kwa sasa imeweka amri ya kutotoka nje nchini kote kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi Alfajiri, hadi angalau tarehe 27 mwezi Julai, ikiwa ni sehemu ya masharti ya kupambana na COVID-19.

Usafiri wa ndani kwenda maeneo ya magharibi mwa nchi pia umepigwa marufuku, hadi angalau tarehe 27 mwezi huu, huku mikusanyiko ya umma, pia ikipigwa marufuku kwa sasa.

Chanzo cha Habari : VOA News / AP

XS
SM
MD
LG