Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:10

Marekani kupeleka kikosi maalum Kenya kukabiliana na ugaidi


Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza kupeleka kikosi maalum cha wanajeshi wa Marekani nchini Kenya.

Gazeti la Sunday Nation la Kenya limeripoti, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters kikosi hicho maalumu ni kwa ajili ya kusaidia eneo hilo katika kukabiliana na ugaidi.

Katika barua yake kwa Bunge la Marekani ambayo gazeti hilo limeiona, Rais Biden amesema kwamba ameidhinisha upelekaji wa kikosi cha operesheni maalum huko Kenya, ambacho kilitarajiwa kushirikiana na jeshi la Kenya katika kupambana na al-Shabaab.

Idadi ya wanajeshi wanaokwenda huko haijatajwa. Upelekaji wa wanajeshi unatarajiwa kuboresha usalama kwa Kenya, ambayo katika miaka ya karibuni imekumbwa na mashambulizi kadhaa kutoka kwa Al shabaab.

Kundi hilo lenye makao yake nchini Somalia linajulikana kuwa lina wanaowaonea huruma nchini Kenya.

Vyanzo vya Habari : Sunday Nation, Reuters

XS
SM
MD
LG