Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 23:08

Somalia yasikitishwa na ripoti za wanajeshi wa Marekani kupangiwa kuondoka


Magari yakichomeka moto baadha ya mojawapo ya shambulizi baya la kigaidi mjini Mogadishu, Somalia. July 30 2017
Magari yakichomeka moto baadha ya mojawapo ya shambulizi baya la kigaidi mjini Mogadishu, Somalia. July 30 2017

Wabunge na maafisa wa kijeshi nchini Somalia wanasema kwamba hatua ya kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini humo itasababisha janga kubwa na huenda ikaliimarisha kundi la Al-shabaab pamoja na makundi mengine ya kigaidi.

Imeripotiwa kwamba rais wa Marekani Donald Trump amependekza kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Somalia.

Katibu wa kamati ya ulinzi katika bunge la Somalia Ahmd Hashi amesema kwamba Marekani chini ya utawala wa Trump, inataka kuiacha Somalia katika kipindi ambacho ni muhimu sana na inapohitaji msaada zaidi.

Hashi ameiambia sauti ya Amerika kwamba nchi hiyo inahitaji msaada wa usalama inapoelekea katika uchaguzi wa bunge mwishoni mwa mwezi Desemba na baadaye uchaguzi wa urais mwezi Februari.

Gazeti la New York Times liliripoti wiki hii kwamba rais Donald Trump anapanga kuondoa wanajeshi 700 wa Marekani nchini Somalia.

Wanajeshi hao wanatoa mafunzo kwa jeshi la Somalia namna ya kukabiliana na ugaidi.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG