Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:31

Somalia na Kenya warejesha mahusiano ya kidiplomasia


Naibu waziri wa habari Abdirahman Yusuf akizungumza na waandishi wa habari mjini Mogadishu, Somalia, May 6, 2021.
Naibu waziri wa habari Abdirahman Yusuf akizungumza na waandishi wa habari mjini Mogadishu, Somalia, May 6, 2021.

Somalia ilitangaza Alhamisi kuwa imerudisha uhusiano wake wa kidiplomasia na Kenya, kufuatia mazungumzo kati ya viongozi wa nchi hizo jirani, waliopatanishwa na Qatar.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Mogadishu, Naibu Waziri wa Habari wa Somalia Abdirahman Yusuf Al-Adala alitangaza, akisema kuwa Somalia inaanza tena uhusiano na Nairobi ambao iliuvunja mwaka jana.

Serikali kuu ya Somalia, "kwa kuzingatia masilahi ya ujirani mwema," yatangaza kuwa imerejesha uhusiano wake wa kirafiki na Kenya, alisema Al-Adala. Makubaliano hayo yalizingatia kanuni za kuheshimiana kwa pande mbili kwa uadilifu wa eneo, kutokuingiliana kwa kila mmoja katika mambo ya ndani, usawa, kunufaishana na kuishi kwa amani.

Al-Adala hakutoa ufafanuzi juu ya jinsi mazungumzo hayo yalianzishwa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili, lakini alisema yalifanyika kwa sehemu kubwa kupitia juhudi za mtawala wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani.

Marais wa nchi zote mbili wanamshukuru mkuu wa Qatar kwa juhudi zake nzuri katika suala hili, "Al-Adala alisema.

Serikali ya Kenya haikujibu mara moja maswali ya VOA kuhusu jambo hili.

XS
SM
MD
LG