Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:17

Bunge la Marekani lavutana juu ya kesi ya Tump


Kutoka kushoto, Kiongozi wa Baraza la Seneti Mitch McConnell, Rais Donald Trump, na Spika Nancy Pelosi.
Kutoka kushoto, Kiongozi wa Baraza la Seneti Mitch McConnell, Rais Donald Trump, na Spika Nancy Pelosi.

Viongozi wa Bunge la Marekani Alhamisi wamezungumzia juu ya hatua zitakazofuatia katika Baraza la Seneti baada ya Baraza la Wawakilishi Jumatano kupiga kura kumfungulia mashtaka Rais Donald Trump, ambaye hivi sasa ni rais wa tatu katika historia ya Marekani kukutikana na makosa.

Katiba ya Marekani inaainisha kuwa Baraza la Seneti ni lazima liendeshe kesi, lakini kuna tofauti kubwa kati ya viongozi wa Wademokrat na Warepublikan katika Bunge kwa kile hasa kingeweza kutokea.

Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na Wademokrat liliidhinisha vifungu viwili vya mashtaka dhidi ya Rais Trump baada ya kukutikana na makosa. Vifungu hivyo ni kutumia vibaya madaraka yake ya urais kujinufaisha yeye binafsi kisiasa na kuzuia juhudi za bunge kuchunguza vitendo vyake. Hakuna Mrepublikan aliyepiga kura kuidhinisha hatua hiyo ya kumshtaki Trump.

Baadae, Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi alikataa kusema wakati gani atawasilisha vifungu vya mashtaka hayo kwenye Baraza la Seneti, akisema ni lazima kwanza aangalie kesi hiyo itakuwa na muono gani.

Mapema Alhamisi, kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell alisimama katika ukumbi wa Seneti na kuwalaani Wademokrat, akisema Pelosi anaogopa kupeleka vifungu hivyo vya mashtaka kwa kile alichokiita “kazi yao iliyofanywa ovyo.” Amesema ni juu ya Baraza la Seneti kusahihisha jambo hilo kwa kumsafisha Trump.

Kiongozi wa waliowachache katika Baraza la Seneti Chuck Schumer alipinga kauli ya kiongozi wa waliowengi, akisisitiza McConnell yeye mwenyewe alieleza hakuwa na dhamira ya kutoegema upande wowote katika kesi hiyo itakayoendeshwa na Baraza la Seneti.

“Ujumbe kutoka kwa kiongozi huyo McConnell kwa wakati huu ni kuwa hana nia ya kuendesha kesi yenye kutenda haki, hakuna nia ya kuwa hanaupendeleo, hakuna nia ya kutafuta ukweli.”

XS
SM
MD
LG