Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:55

Rais Trump awashambulia wademokrats baada ya kumfungulia mashtaka bungeni


Wabunge wa baraza la wawakilishi wapiga kura kumfungulia mashtaka Rais Trump. Jumatano, Dec. 18, 2019, bungeni Washington. (AP Photo/Patrick Semansky)
Wabunge wa baraza la wawakilishi wapiga kura kumfungulia mashtaka Rais Trump. Jumatano, Dec. 18, 2019, bungeni Washington. (AP Photo/Patrick Semansky)

Rais Donald Trump amezungumza kwa hasira katika mkutano wa kisiasa baada ya Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani kupiga kura na kumfungulia mashtaka, Jumatano usiku.

Katika tukio la kihistoria wabunge wa chama cha Demokratik kwa karibu sauti moja wamemfungulia rais Trump mashtaka mawili, ya kutumia vibaya madaraka yake kuhusiana na kadhia ya Ukraine na kuzuia mkondo wa sheria za bunge kufanya kazi.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani kwa rais kufunguliwa mashtaka akiwa katika mhula wake wa kwanza na Trump anakua pia rais wa tatu kufunguliwa mashtaka.

Wakati wabunge walipokua wanajadili kumfunguliwa mashtaka hayo, rais Donald Trump alikua ana wahutubia wafuasi wake sugu 7,000 katika mji wa Battle Creek, jimbo la Michigan ambako kuna ushindani mkubwa kati ya chama cha Republican na Demokratik.

Katika hotuba yake iliyokua ndefu kabisa ya kampeni, iliyodumu saa mbili Trump alizungumza kwa hasira, ucheshi na kukaidi matokeo, akisema ni njama ya wademokrats ya kutaka kumondowa madarakani.

“Wademokrats watangaza chuki zao za dhati na kudharua maoni ya wapiga kura wa Marekani,” alisema Trump akishangiriwa na wafuasi wake.

Aliongeza kusema kwamba, “wamekua wakijaribu kunifungulia mashtaka tangu siku ya kwanza. Wamejaribu kunifungulia mashtaka hata kabla sijaanza kugombania nafasi hii.”

Kesi kufunguliwa mwakani

Hivi sasa mashtaka hayo yanabidi kufikishwa mbele ya Baraza la Senat, ambako kesi itafunguliwa kuhusiana na mashtaka ambayo yanaweza kumsababisha kuondolewa madarakani.

Lakini katika tukio ambalo halikutazamiwa, Spika wa Baraza la Wawakilishi Nacy Pelosi, akizungumza na waandishi habari baada ya kumfungulia mashtaka Trump, alisema huwenda akachelewesha kupeleka mashtaka hayo kwenye baraza la senate.

Spika Nancy Pelosi akizungumza na waandishi habari baada ya kumfungulia mashtaka Trump
Spika Nancy Pelosi akizungumza na waandishi habari baada ya kumfungulia mashtaka Trump

“Hadi hivi sasa, hatujaona kitu chechcote kinacho fananan na utaratibu wa haki kwetu sisi. Hivyo tuna matumaini itakuwa ya haki zaidi, na hapo tutawatuma wajumbe wetu na mashtaka hayo,” alisema Pelosi.

Wachambuzi wanasema msimamo huo wa spika unatokana na matamshi ya maseneta wa chama cha Republican kwamba wataharakisha kesi na hawataruhusu mashahidi.

Hata ikiwa kutakuwepo na kesi ya haki, wachambuzi wanasema haiaminiki warepublican watapiga kura kumondowa rais mashuhuri, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu.

Warepublican wanaolilidhibiti Baraza la Senate wameungana kabisa nyuma ya Trump na haiaminiki watapiga kura kumondowa. Wademokrats watahitaji maseneta 20 wa chama cha Republican kuungana nao kuweza kumondowa.

Kesi hivi sasa inatazamiwa kuanza wakati wowote mwakani baada ya Pelosi kuamua cha kufanya.

XS
SM
MD
LG