Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 14:33

Wagombea urais saba Wademokrat wamshambulia Trump kuwa fisadi


Mdahalo wa chama cha Demokrat uliofanyika Los Angeles, California, US Disemba 19, 2019. REUTERS/Kyle Grillot
Mdahalo wa chama cha Demokrat uliofanyika Los Angeles, California, US Disemba 19, 2019. REUTERS/Kyle Grillot

Wagombea saba wanaoshika hatamu kuwania nafasi ya urais katika mchakato wa chama cha Demokrat kwa pamoja waliungana, katika mdahalo uliokuwa wa nguvu jioni Alhamisi, haraka kumshambulia Rais Donald Trump ambaye amekutikana muda siyo mrefu na hatia, wakisema kuwa ni kiongozi fisadi zaidi katika historia ya Marekani.

Wagombea wote wanaotaka kuteuliwa kupitia chama cha Demokratic kukabiliana na Trump katika uchaguzi wa taifa mwaka 2020 wamesema wanaunga mkono hatua ilichukuliwa masaa 24 yaliyopita na Baraza la Wawakilishi vifungu viwili vya makosa yanayomtuhumu Trump kuwa alitumia vibaya madaraka yake ya urais kujinufaisha yeye binafsi kisiasa na kuzuia Bunge kufanya kazi yake.

“Tunahitaji kurejesha hadhi ya ofisi ya urais,” amesema Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden, mgombea aliye endelea kushika nafasi ya mbele katika kura za maoni za Wademokrat wanaowania kuteuliwa katika kinyang’anyiro hicho.

Baadae, Biden, akitoa maoni yake juu ya mgawanyiko wa kina wa kisiasa nchini Marekani kati ya Warepublikan na Wademokrat ambao umeendelea kuongezeka katika kipindi cha miaka mitatu Trump akiwa madarakani, amesema, anakataa “kukubali juu ya ukweli wa kuwa hatuwezi kujumuika pamoja tena.”

Seneta Bernie Sanders wa Vermont, Mdemokrati aliyechagua yeye mwenyewe kuwa msoshaliti aliyekuwa nyuma ya Biden katika kura nyingi za maoni, amesema Trump “msema uongo mzoefu” ambaye amewauza wafanyakazi wa nchi.”

Seneta Elizabeth Warren wa Massachusetts amemuelezea Trump kama “rais fisadi zaidi katika karne.”

“Rais huyu siyo mfalme wa Marekani,” Seneta Amy Klobuchar wa Minnesota amesema. Amefananisha vitendo vya Trump vya kutaka Ukraine kumchunguza Biden na mtoto wake na kashfa ya ufisadi wa kisiasa ya Watergate mwaka 1970 iliyopelekea Rais Richard Nixon kujiuzulu akikabiliwa na kufunguliwa mashtaka.

XS
SM
MD
LG