Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 16:32

Mdahalo wa Wademokrat wagubikwa na suala la Ukraine


Wagombea watatu Wademokrat wanaoongoza katika kinyang'anyiro cha urais Seneta Bernie Sanders, kushoto, Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden na Seneta Elizabeth Warren,kulia, wakishiriki mdahalo, Jimbo la Ohio.by CNN/New York Times at Otterbein…

Mgombea kiti cha urais wa chama cha Demokratic Seneta Elizabeth Warren anayeongoza hivi sasa miongoni mwa wagombea 20 wa chama hicho alishambuliwa vikali na wenzake Jumanne usiku wakati wa mdahalo wa kitaifa.

Seneta huyo alikosolewa kutokana na sera zake za msimamo mkali wa mrengo wa kushoto kuhusu huduma za jamii na afya na kuongeza kodi kwa matajari wa Marekani ili kuweza kukusanya fedha kugharimia miradi ya kijamii.

Seneta huyo hata hivyo aliweza kujibu mashambulizi hayo na kuimarisha nafasi yake kama mgombea anayetarajiwa kupambana na Rais Donald Trump katika uchaguzi wa rais 2020.

Suala kuu lililojitokeza la kufunguliwa mashtaka rais kutokana na kadhia ya Ukraine ya kumtaka rais wa nchi hiyo kufanya uchunguzi dhidi ya Joe Biden, huku wagombea wakimshambulia rais kwa kuondoa wanajeshi wa Marekani Syria jambo lililosababisha uturuki kushambulia maeneo ya Wakurdi kaskazini mwa nchi hiyo.

Seneta Warren akichangia katika mdahalo huo amesema kufunguliwa mashtaka dhidi ya Trump ndio njia "ya sisi kudhihirisha kwamba mtu huyu hataruhusiwa kuvunja sheria mara kwa mara bila ya kuadhibiwa."

Nyota wa mdahalo huo ulowashirikisha wagombea 12 alikuwa meya wa mji mdogo wa South Bend Pete Buttigieg aliyeshambulia sera za Trump kuhusu Syria, na kushindana vikali na wenzake kuhusu bima ya afya kwa wamarekani wote, udhibiti wa bunduki na masuala ya kigeni.

Wademokrats watakuwa na mdahalo wao ujao mwezi Novemba jimboni Georgia.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG