Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 12:50

Mwanasheria Mkuu Barr akosolewa anavyosimamia habari zilizovuja


Mwanasheria Mkuu William Barr
Mwanasheria Mkuu William Barr

Mnamo mwezi Machi, mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller aliwasilisha ripoti yake ya mwisho kwa Mwanasheria Mkuu William Barr bila ya kujibu maswali yenye kutatanisha : Iwapo Rais Donald Trump alijaribu kuzuia uchunguzi usifanyike kujua iwapo Rashia iliingilia kati uchaguzi wa urais mwaka 2016 kwa ajili ya kumsaidia Trump ashinde uchaguzi huo.

Hivi sasa Barr amejikuta yuko ndani ya mgogoro mwengine mzito uliomfunika rais huyo : malalamiko makali yaliovujishwa na afisa wa usalama akisema kwamba Trump aliishinikiza Ukraine kuchunguza dosari za kisiasa dhidi ya mgombea urais wa chama cha Demokrat aliyeko mstari wa mbele Joe Biden na mtoto wake, Hunter Biden.

Pamoja na kuwa uchunguzi umelenga mazungumzo ya simu ya Trump aliofanya Julai 25 na maafisa wa White House katika juhudi zao za kuzuia maelezo ya kina ya mazungumzo hayo, wabunge wa Chama cha Demokrat wanamkosoa zaidi Barr kule kujihusisha kwake katika suala hilo na namna Idara ya Sheria inavyoshughulikia malalamiko ambayo yako chini yake.

Barr, Wakili mahiri mzoefu Mrepublikan, ilipotoka ripoti ya mwendesha mashtaka Mueller hakupoteza muda wowote kujibu swali hilo kwa umma : Yeye na naibu wake walihitimisha kwamba hakuna ushahidi wa Trump kuzuia uchunguzi. Mbinu alizotumia Barr zilizuwa ukosoaji kwa Wademokrati. Lakini hatua ile ilimwezesha Trump kudai kuwa yeye alikuwa hajakutikana na kosa lolote katika uchunguzi huo.

Wakati wa mazungumzo hayo, Trump alirejea mara kadhaa kumshinikiza Zelenskiy kuzungumza na Barr na wakili wake Trump, Rudy Giuliani, “ili kupata taarifa za ndani” za madai ya makosa waliotenda huko Ukraine familia ya Biden ambayo hayakuthibitishwa. Trump wakati huohuo alisisitiza jinsi gani Marekani imeipatia Ukraine msaada wa kijeshi.

White House ilitoa waraka wa Rais Donald Trump wa Julai 25, 2019, uliokuwa na mazungumzo ya simu aliyofanya na rais mpya wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy.

Barr ametajwa mara kadhaa katika malalamiko yaliyoko katika kurasa tisa na waraka wa White House wa Julai 25 wa mazungumzo ya simu kati ya Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy.

Madai hayo yaliyokuja kwa ghafla yamepelekea Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi wiki hii kutoa amri ya kuchunguzwa rasmi mwenendo wa Trump ikiwa ni mchakato wa kutaka kumuondoa katika madaraka ya urais.

XS
SM
MD
LG