Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 04:03

Upinzani wa wananchi unapata nguvu Libya


Watu wakiimba na kubeba mabango yanayotwa wito wa kufanya migomo hadi kuanguka kwa utawala wa Ghadafi.
Watu wakiimba na kubeba mabango yanayotwa wito wa kufanya migomo hadi kuanguka kwa utawala wa Ghadafi.

Mashahidi katika mji mkuu wa Libya wanasema majengo ya serikali yametiwa moto na wanaharakati wa upinzani wanaopambana na vikosi vya usalama

Upinzani wa wananchi dhidi ya utawala wa kiongozi wa muda mrefu wa Libya Moammar Gadhafi unaendelea kupata nguvu, wakati mashahidi wakisema kuna baadhi ya majengo ya serikali katika mji mkuu wa Tripoli yametiwa moto na wanaharakati wa upinzani wanaopambana na vikosi vya usalama.

Mashahidi wanasema majengo yaliwaka moto baada ya mapigano ya bunduki kuzuka Tripoli Jumapili usiku kwa mara ya kwanza, pale wandanmanaji wanaoipinga serikali kujaribu kuchukua udhibiti wa eneo la kati la mji lililokua linashikiliwa na wafuasi wa Ghadafi.

Kijana wa Ghadafi Saif al-Islam alizungumza kwa mara ya kwanza kwenye televisheni ya Taifa siku ya Jumpaili akidai kwamba babake anaendelea kuwa kiongozi na jeshi linamunga mkono wakati wa malalamiko haya mkubwa kabisa kuwahi kutokea tangu kuchukua madaraka 1969.

Saif sl-Islam ameapa kwamba serikali itapambana hadi mwanamume wa mwisho, mwanamke wa mwisho, na risasi ya mwisho ili kubaki madarakani.

XS
SM
MD
LG