Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 08:23

Wamisri wafurahia mwisho wa Mubarak


Wamisri wakisherekea kuondoka madarakani kwa Hosni Mubaraka mjini Cairo

Kujiuzulu kwa Rais Hosni Mubarak kumehamasisha maelfu kwa maelfu ya watu kukimbilia katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo Ijumaa. Watu walicheza dansi, kushangilia na kutoa machozi ya furaha baada ya madai yao ya siku 18 za maandamano kukubaliwa na uongozi wa karibu miaka 30 wa Hosni Mubarak kufikia kikomo.

"Yamekwisha. Taifa limemaliza uongozi huu." Maneno hayo yalitolewa na wazee kwa vijana, wake kwa waume na watoto waliokuja nao katika uwanja huo kusherehekea mabadiliko yaliyotokea Misri.

"Karibu, karibu katika Misri mpya." Maneno kama hayo yaliashirikia furaha ya kumalizika kwa enzi moja na kuanza kwa enzi nyingine nchini Misri.

Jeshi ambalo limechukua madaraka linaahidi kulinda taifa hilo, ikiwa kama mwangwi wa asili ya utaifa uliomalizika Ijumaa. Si kila mahali wananchi wanakaribisha jeshi kuchukua madaraka lakini hivyo ndivyo ilivyo Misri katika karne iliyopita, pale Gamal Abdel Nasser aliposaidia kupindua ufalme na kuwaambia wananchi wa Misri"inueni sura zenu."

XS
SM
MD
LG