Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:41

Mgogoro Misri waathiri biashara Kenya


Maelfu ya tani za chai yamekwama katika bandari ya Mombasa ikisubiri safari kwenda Misri
Maelfu ya tani za chai yamekwama katika bandari ya Mombasa ikisubiri safari kwenda Misri

Mgogoro wa kisiasa unaoendelea Misri umeanza kusababisha hasara za kiuchumi na kibiashara nchini Kenya. Baadhi ya wafanyabiashara na wakulima Kenya wanafuatilia mgogoro huo kwa makini wakitumaini kuwa utamalizika haraka na kurejesha biashara baina ya Kenya na Misri.

Kulingana na Bodi ya majani ya chai, Kenya kiwango cha chai kinachouzwa nchini Misri kinazidi kupungua kwa haraka. Mwaka uliopita Kenya iliiuzia Misri kilo millioni 390 za chai lakini kiasi hicho kinapungua kwa karibu asilimia 40.

Mwaka huu pekee Kenya imeuzia Misri kilo milioni 93 zqa chai kabla ya kuzuka kwa mgogoro wa kisiasa Misri. Bodi ya chai inasema kuna kiwango kikubwa cha chai kilichokwama katika bandari ya Mombasa ikisubiri kusafirisha kwenda Misri.

Zao la chai ni moja ya mazao makubwa ya biashara yanayotegemewa kuingiza fedha za kigeni katika uchumi wa Kenya.

XS
SM
MD
LG