Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 07:16

Marekani yaonyesha tahadhari Misri


Umati wa watu waliojazana katika uwanja wa Tahriri mjini Cairo kwa maandamano ya amani Februari 1, 2011.
Umati wa watu waliojazana katika uwanja wa Tahriri mjini Cairo kwa maandamano ya amani Februari 1, 2011.

Marekani inaonyesha hatua za tahadhari katika kufuatilia mzozo unaoendelea huko nchini Misri ambapo wananchi wa nchi hiyo wameendelea kumshinikiza Rais Hosni Mubarak kuachia madaraka.

Profesa Julius Nyang’oro wa chuo kikuu cha North Carolina hapa Marekani amesema kuwa serikali ya Marekani hivi sasa inayafuatilia maandamano ya nchini Misri kwa hali ambayo isingependa ilazimishe mabadiliko ya haraka, wakati ambapo hakuna uongozi ambao umeibuka na unaonekana unaweza kushika hatamu za uongozi wa nchi, hali ambayo inaweza kuleta dosari kwenye uhusiano kati ya nchi hizo.

Profesa Nyang’oro ameongezea kwamba uhusiano wa muda mrefu baina ya Marekani na Misri si jambo ambalo linaweza kufutwa ghafla bila ya kutafakari. Amesema lakini katika siku chache zilizopita serikali ya Marekani imeonyesha ishara kwamba mabadiliko yatatokea nchini humo lakini hili halitafanyika haraka sana kama vile ambavyo wananchi wa misri wanavyotaka.

Kuhusu uhusiano wa Marekani na wananchi wa Misri, Profesa Nyang’oro amesema imedhihirika wazi kuwa watu wa Misri wanaichukulia Marekani kuwa ni rafiki na mshirika, na hili limejionyesha katika maandamano na kwenye baadhi ya mabango ambayo yameandikwa “tafadhali Marekani usiwaudhi watu wa Misri kwa kuisaidia serikali iliyopo madarakani”.

XS
SM
MD
LG