Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 11:57

Viongozi wa chama tawala Misri wajiuzulu


Waandamanaji mjini Alexandria wakimba nyimbo za kuipinga serikali na kumtaka Rais Hosni Mubarak kuondoka huko Misri.
Waandamanaji mjini Alexandria wakimba nyimbo za kuipinga serikali na kumtaka Rais Hosni Mubarak kuondoka huko Misri.

Maelfu na maelfu ya wandamanaji walijitokeza tena Jumamosi katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo, na miji mbali mbali ya Misri katika juhudi za kumtaka Rais Hosni Mubarak aondoke madrakani.

Wakati huo huo inaonekana kiongozi huyo anachukua hatua za kujiondowa, ilipotangazwa Jumamosi kwamba anaacha uwongozi wa chama chake cha National Democratic Party NDP, pamoja na viongozi wote wa juu wa chama hicho ikiwa ni pamoja na kijana wake Gamal.

Wandamanaji kwa siku ya 12 mfululizo walikusanyika kwenye uwanja wa Tahriri na kumeleza kiongozi wao mwenye umri wa miaka 82 kwamba hawataondoka hadi atakapoacha madaraka.

Baadhi ya wandamanaji walisherehekea tangazo la mabadiliko katika chama tawala lakini walisema malalamiko yataendelea.

Kwa upande mwengine wafanya bishara wameanza kueleza wasi wasi wao juu ya lini maisha yatarudi kuwa ya kawaida, na wa Misri wengine wakisema malalamiko yamesikika na maisha yanabidi kurudi kuwa ya kawaida.

Vyombo vya habari na wachambuzi wa mambo wanasema mungano wa vyama vya upinzani na wawakilishi wa waandamanaji wamekubali kuanza majadiliano na serikali juu ya utaratibu wa kuanza mpito kuelekea mfumo wa kweli na thabiti wa kidemokrasia huko Misri.

XS
SM
MD
LG