Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:28

Viongozi wa dunia watoa wito wa utulivu Misri


Waandamanaji wa Misri wakimba nyimbo kumtaka rais Mubarak kuondoka mara moja.
Waandamanaji wa Misri wakimba nyimbo kumtaka rais Mubarak kuondoka mara moja.

Rais Barack Obama ametoa wito wa kuwepo na kipindi cha mpito kitakachopelekea kundwa serikali itakayo sikiliza matakwa ya wananchi. Viongozi wa Ulaya kwa upande wao wametoa wito wa kuwepo na uchaguzi wa huru na haki katika taifa hilo la Kiarabu lenye wakazi wengi.

White House ilieleza Jumapili kwamba rais Obama alizungumza na viongozi wa Uingereza, Uturuki, Israel na Saudi Arabia mnamo siku mbili zilizopita. Alirudia nia ya serikali yake ya kuwepo hali ya kustahmiliana wakati inaunga mkono haki za kidemokrasia kwa wananchi wa Misiri ikiwa pamoja na haki ya kukusanyika pamoja kwa amani na haki ya kujieleza.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Florida Charels Bwenge anasema Marekani inajikuta katika hali nzito, kwa upande haiwezi kumtupa rafiki yake wa muda mrefu katika utaratibu wa amani na wakati huo huo inaunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia kwa wamisri.

Viongozi wa nchi za Kiarabu wamekua wakitoa maoni yanayotafautiana juu ya hali huko Misri, baadhi wakiunga mkono utawala wa Cairo wengine wakitoa mwito wa mabadiliko ya amani.. Viongozi wa Saudi Arabia wamempelekea rais Mubarak ujumbe wa kumunga mkono, huku Iran ikiwa unga mkono wananchi kama anavyoeleza mwandishi habari Abdallah Wachu.

Licha ya ghasia zilizoshuhudia mnamo siku tano za mandamano na uwasi wa wananchi dhidi ya utawala wa muda mrefu wa Mubarak, viongozi wa upinzani wa Misri pamoja na wananchi kwa ujumla wangelipendelea mabadiliko ya amani na kumtaka Mubarak kuondoka mara moja.

XS
SM
MD
LG